Wanachama wa Namaingo Agency wakinukisha kwa DC Mjema, wamtaka Mkurugenzi wao kukamatwa kwa utapeli

WANACHAMA wa Kampuni NAMAINGO BUSINESS AGENCY iliyoko Kata ya Ukonga Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambayo inajihusisha na a masuala ya ushauri wa biashara, ujasiriamali na utekelezaji wa uatamizi wa wajasiriamali kwa kuwapa elimu ya kilimo hususani kilimo biashara na kuwaunganisha na fursa zilizopo ikiwamo utaalamu , Masoko na Mitaji  katika kujikwamua kiuchumi  , leo wamefika kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema, kupeleka malalamiko dhidi ya mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya utapeli .

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo asubuhi Ofisini kwake, DC Mjema, amesema kuwa hawawezi kuvumilia utapeli kama huo katika Wilaya yake, hivyo ametoa agizo la kumtaka Mkurugenzi huyo kufika Ofisni kwake mara moja kesho asubuhi kwa ajili ya mahojiano akiwemo RPC  na endapo atakiuka wito basi jeshi la Polisi litawajibika kumkamata mara moja ili kumfungulia mashtaka endapo madai ya Wanachama hao yatakuwa na ukweli ndani yake.

"Nataka kuwahakikishia ndugu zangu, mimi nimeteuliwa na Rais kuwatumikia wana Ilala hivyo watu wanaotaka kula  kwa kutumia nguvu za watu wengine katika wilaya yangu hawana nafasi, niseme kuwa huyu Mkurugenzi  namtaka afike hapa kesho saa 2:00 asubuhi na nyinyi mkiwepo ili kubaini ukweli wa jambo hili na kama atabainika tutamshuhurikia mara moja na kumungulia mashtaka"amesema DC Mjema


Naye aliyekuwa Mkurugenzi wa miradi katika Kampuni hiyo, Amos Misinde, amesema kuwa aliamua kuachana na Kampuni hiyo mara baada ya kugundua haina mipango ya dhati ya kuwasaidia Wanachama wake na sio kuukuzwa kazi kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti awali pamoja na Mkurugenzi wa Namaingo alivyo sema .

Amesema kuwa, Mkurugenzi huyo alikuwa akifanya kazi za kiutapeli bila wao kujijua hivyo katika hali ya utendaji kazi bila mafanikio huku akibuni miradi mbali mbali ambayo ilikuwa haina tija kwa Wanachama wake, ndipo walipogundua kuna upigaji unaendelea baina ya Kampuni hiyo.

Misinde, amesema kuwa wakati wanajiunga katika Kampuni hiyo mwaka 2016, waliahidiwa kwamba wakijiunga Mradi wa Kijiji biashara wangeweza kupatiwa kiasi cha Shilingi 200,000,000 kwa mwaka wa kwanza kama faida ghafi, hivyo kitu ambacho kiliwavutia Watu wengi nakuwafanya kujiunga huku wakijawa na matumaini lukuki katika kujikwamua kiuchumi .

.

"Tulipewa matumaini makubwa sana kwamba ndani ya muda mfupi kila mtu atakuwa na pesa za kutosha , hadi leo ni mwaka wa tatu sasa hakuna hata kitu kimoja ambacho Wanachama waliahidiwa kilifanyika, ndio maana tuliamua kuiandikia barua Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) kutaka kujua ni lini Mradi wa Kijiji Biashara utatekelezeka maana ni mwaka wa tatu sasa bila mafanikio , maana wakati tuna hamasishwa kuhusu mradi huu tuliambiwa kuwa NEEC linashirikiana na Kampuni ya Namaingo kuhakikisha kuwa Mradi huu unatekelezeka bila wasi wasi wowote"amesema Misinde.

Katika hatua nyingine, Renalda Mrema, ambaye ni Mwanachama wa Namaingo na miongoni mwa waathirika , ameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo ili huyo mama asiendelee kuwatapeli watu wengine ambao bado hawajajitambua na ufumbua macho, kwani waliahidiwa kusoma SIDO , Mmboga mboga kwa kulipia pesa lakini mwsho wa siku hakuana hata lililofanyika zaidi ya kuibiwa na kumnufaisha mtu mmoja .



Stori hii itaendele kesho ili kujua hatma ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kuhusu shutuma zinazomkabili dhdi ya Wanachama wake.

Related

habari 8735009608252939314

Post a Comment

emo-but-icon

item