Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir yahusishwa na utapeli wa nyumba upanga

TAASISI  moja  ya dini inayofahamika kwa jina la Khoja Shia Ithna-asheir , wamevamia nyumba yenye namba 868 ya mkazi mmoja anyejulikana kwa jina la Edith Max iliyoko Upanga bara bara ya Mfaume Kata ya Upanga Magharibi huku wakidai wao ndio wamiliki halali wa Nyumba hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mapema katika eneo hilo la tukio, Edith Max, ambaye ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo mara baada ya mumewe kuachiwa urithi huo  na baba yake mzazi aliyetangulia mbele za haki.

Edith ,amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo hadi kufikia Nyumba hiyo kuvamiwa ni kutokana na mtoto mmoja wa marehemu ambaye jina lake lilihifadhiwa kwenda kukopa kiasi cha Shilingi Milioni 30, kwenye benki ya Furaha kabla ya kubadilishwa jina ambapo kwa sasa inajulikana kwa jina la CUF Benki .
Image may contain: 1 person
Aidha, mama huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa uchungu mkubwa sana, amesema mkopo huo ulikuwa sio halali kwani mtu huyo alichukuliwa kitapeli na watu waliojifanya ni wasimamizi wa mirathi  na kumwambia kama atakopa fedha hizo atapatiwa licha ya mirathi kufunguliwa.
Image may contain: outdoor
Amesema kuwa, baada ya mkopo huo ambapo hati ya nyumba hiyo ilipelekwa Mahakamani  na Benki hiyo , hivyo waliambiwa  ili wapatiwe hati hiyo lazima walipe deni  lao  benki lakini cha kushangaza katika ufuatiliaji wa malipo hayo benki hiyo ilikuwa ikiwazungusha pasipo na sababu za msingi huku wakidai tozo ya riba imepanda hadi kufikia Milioni 120.
Image may contain: outdoor
Mama huyo alienda mbali zaidi akisema kuwa, baada ya agizo hilo la malipo wao walikuwa tayari kulipa lakini kila wanapofika Benki  wamekuwa wakisumbuliwa hadi kufikia watu hao kuwakimbia jambo ambalo lilileta sintofahamu kati ya Benki hiyo na wateja hao kwani mlengo wao ulikuwa ni kuwauzia watu wengine nyumba hiyo.

"Tumefuatilia sana benki ili kulipia malipo lakini wamekuwa wakitukimbia kila wanapotuona na kutupandishia  gharama ili tushindwe kulipa wao wafanye utapeli wao, tumefuatilia kesi mahakamni mara tano bila majibu ya kueleweka, hivyo tuliposikia mkuu wa Mkoa Mh: Paul Makonda akitangaza kuwasaidia wale walidhurumiwa na wenye changamoto ya ardhi tulifikisha kesi hiyo na kusikilizwa pande zota na Makonda kuamuru jarada hilo lifuatiliwe lakini jana wakati tukijaribu kufuatilia jarada letu kwa makonda watu hao walivamia nyumba hiyo na kuanza kuvunja huku wakisema hawamuogopi makonda wao serikali wameishika hivy tulipambana nao hadi askali waliingilia kati na kufunga jengo hili" amesema  Edith

"Inauma sana ndugu waandishi, maisha yangu yamekuwa ya kutanga tanga, nimekuwa mtu wa kusaidiwa mimi watoto zangu wanalipiwa kodi ndugu wanajichanga kuhakikisha naishi vizuri, mume wangu amepalalaizi mguu matibabu makubwa tunahangaika kila kona maisha yangu yapo hatarini kwa sasa kwani kuna watu wananifuatilia kwa sasa sina amani kabisa naomba serikali inisaidie ikiwezekana ulinzi nuwepo katika familia yetu, Rais  wa wanyonge Magufuli unatusikia, Makonda pigania hili mungu amekupa kipawa cha kuwatumikia wananchi, tupambanie tuna teskea sana baba"alizidi kuongeza mama huyo

Katika hatua nyingine, msimamzi wa mirathi hiyo, Max Kafipa, amesema watu hao sio mara ya kwanza kufanya matukio hayo ya kutapeli maeneo bali imekuwa ni kama kazi zao na walishafanya matukio hayo mara nyingi sana, lakini alisema katika kuonyesha  wao atukikubali kwani hata benki nayo imefanya utapelei wa kupiga mnada nyumba yetu bila kutushirikisha ambapo ni kinyume na sheria.

"Mimi ndiye msimamizi halali wa nyumba hii, katika eneo hili tulikuwa na nyumba sita ambapo nyingine tulipangisha kwa wanafunzi wa chuo cha mzumbe, lakini tunashangazwa sana na matapeli hawa wamefanya vitu vya ovyo sana, hapa kuna mikono ya watu wengi eneo hili walilitaka kwa muda mrefu hivyo wameona kutumia mabavu yao walipate kiurahisi kwani hata huko mahakamani hizo hati zilizokuwa zikitumika zilikuwa feki kuanzia wasimamizi hadi wahisika wa mnada huo ikiwamo benki na taasisi ya Khoja Shia Ithna-asheir    "amesema Kafipa

Kwa mujibu wa msimamizi wa mirathi, Kafipa amesema mirathi rasmi ilifunguliwa mnamo tarehe 17/1/2018, hivyo kitendo cha kununua Nyumba yetu kwa shilingi milioni 800 ni kinyume na sheria .

Ametoa wito kwa Serikali huku akimuomba Rais magufuli, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na Waziri wa ardhi waingilie kati mgogoro huo shida  yao ni kuona mali yao inarudioshwa kwenye mikono yao salama kwani kitendo cha kutolewa nje mwaka 2014  Agusti tarehe 7 kilipelekea kupoteza maisha ya mama mzazi wa emanuel Max ambaye ndiye mume wa mama Edith na mtoto wa marehemu ambaye aliiacha nyumba hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

item