Tambua faida za Boga

BOGA ni moja kati ya matunda yenye faida mbalimbali katika mwili wa binadamu. Hupatikana karibu mikoa yote ya Tanzania, na idadi kubwa ya watu wengi kulima boga kwa matumizi ya nyumbani kama chakula.
Wengi pia hawajui faida za tunda zaidi ya kulitumia kama chakula, lakini ukweli ni kwamba matumizi yake ni zaidi ya chakula.
Boga huweza kusindikwa au kusagwa na kupatikana kimiminika (juisi) muhimu kwa afya ya binadamu kwani hutibu magonjwa mbalimbali.

Dk. Othman Shemu ni mtaalamu wa miti na mimea dawa na Mkurugenzi mtendaji wa kliniki ya tiba asili cha Paseko yenye makao yake Tabata relini Jijini Dar es Salaam, anasema juisi ya boga pia huimarisha na kuongeza nguvu za kiume.

Huwafanya wanaume kumudu tendo la ndoa hasa wale ambao huishia mshindo au pigo moja au kushindwa kumfikisha kileleni mwanamke na wakati mwingine kukosa hamu ya tendo la ndoa Anasema tunda la boga lina protini na virutubisho mbalimbali vyenye uwezo wa kutibu magonjwa ikiwamo kutengeneza mbegu za kiume kwa wingi kama ilivyo baadhi ya vyakula vya protini.

Baadhi ya magonjwa hayo ni tezi dume, kusafisha figo, tatizo la kutapika mfululizo hasa kwa mama mjamzito, huondoa tatizo ya gesi tumboni na msongo wa mawazo.
“Ukitunia juisi hii huruhusu ubongo kuingiza hewa safi kwa wingi (oxgen) na kutoa hewa chafu hali inayofanya ubongo kuwa mwepesi na kutunza kumbukumbu za kutosha, “ anasema Dk Shemu.

Pia huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuondoa vijidudu visivyotakiwa tumboni, pamoja na kusaidia kurekebisha mfumo wa msukumo wa damu kwa watu wenye matatizo ya presha.

Huweza kutumiwa na rika za watu wote ingawa ni muhimu zaidi kutumiwa na watoto kwani huwakinga na magonjwa na kuwasaidia kujenga uwezo wa kufikiri na kutunza kumbukumbu (akili) jambo ambalo linaweza kuongeza ustawi wa masomo darasani.
UANDAAJI:

Shemu ambaye pia ni katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Waganga (SHIVYATIATA) anasema zipo njia mbalimbali za uandaaji wa ambapo mhussika anasema kumenya maganda ya juu yasiyotakiwa kisha maandalizi kuanzia nyama (sehemu ya njano), moyo na mbegu.

Chukua nyama, kata vipande vidovidogo baada ya kusafishwa kwa maji safi na salama. Jaza vipande hivyo kwenye mashine maarufu kama (Brenda) kwa ajili ya kusaga au kusindika.

Unaweza wakati wa kusindika unaweza kuchanganya vipande hivyo na ndizi, maji safi kidogo ili kurahisisha usindikaji kutokana na ndizi na vipande vya boga kuwa katika hali kavu.

Inashauriwa kuwa juisi iliyosindikwa katika mchanganyiko huo ina ongezeko kubwa la virutubisho kama vile kalishiamu husaidia watu wenye upungufu au ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuongeza kinga ya mwili.

“Pia majaribio yetu yameonyesha kwamba juisi hii ikichanganywa na juisi ya maua yajulikanayo kama rosemary maarufu kama rosella inakuwa na uwezo zaidi katika tiba kutokana na virutubisho vingine kama kalishiam na magnesiamu vilivyomo kwenye rosella,”alisema.

Zipo aina mbalimbali za uandaji wa juisi ya boga kwa mtu mwenye tatizo la nguvu za kiume hutakiwa, kuchukua boga na kulikata vipande vidogo vidogo na kusaga bila vipande hivyo kuwa mbegu zake.

Anachotakiwa mhusika kufanya ni kuzipaa mbegu za boga ili kuzitenganisha na nyama kisha kuzianika sehemu yenye kivuli hadi zitakaponyauka, saga kwa ajili ya kupata unga.

Inashauriwa kusaga unga huo wakati wa matumizi tu kwani unga wake ukihifadhiwa muda mrefu unaweza kusababisha mlundikano wa fangasi ambao ni hatari kiafya, alisema Dk. Shemu.

MATUMIZI:
Unaweza kunywa juisi ya boga iliyosindikwa na kuchanganywa na pensheni ili kuongeza ladha (test) na sukari kidogo kadri unavyoweza kwasababu matumizi yake mengi hayadhuru.

Kuhusu unga wa mbegu za boga, mtumiaji mwenye matatizo hayo anatakiwa kuchukua unga kwenye kijiko kimoja cha chai kisha kuchanganya kwenye glasi ya maji na kunywa.


“Kunywa mara tatu kwa siku. Mwneye tatizo kubwa anapaswa kunywa katika muda wa siku 21 mfululizo. Kwa mwenye tatizo la msongo wa mawazo anaweza pia kunywa juisi ya mchanganyiko wa ndizi mbivu na boga kwa kuchanganya na unga wa mbegu hizo”alisema.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia website Tweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

LISHE 1456467994485518611

Post a Comment

emo-but-icon

item