Sanga awashusha pumzi Yanga kuhusu uwekezaji

Siku kadhaa baada ya Simba kumtangaza Bilionea Mohammed Dewji kama mshindi wa zabuni iliyotangazwa na kumfanya Mo kuwa mshindi wa umiliki wa Hisa asilimia 49 ndani ya klabu ya Simba , Uongozi wa Juu Yanga nao wazungumza kuelekea Mabadiliko.

Image result for clement sanga yanga
Kaimu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga  ambaye ndiye mwenyekiti kikatiba kutokana na aliyekuwa mwenyekiti Yusuph Manji  kujiuzulu amesema Yanga katiba yao inawaruhusu kufanya mabadiliko ya kuruhusu kampuni kuanzishwa ndani ya Yanga na Yanga kumiliki kampuni hiyo.

Sanga amesema katiba yao imeeleza juu ya suala hilo na ni katiba ya toka mwaka 2010  na serikali imeshatoa mwongozo kwahiyo mapema Sana Sanga ameahidi atakaa na kamati ya utendaji kuridhia na kisha watakaa kujadili na kuunda kamati itakayoshugulikia mchakato mzima wa mabadiliko ndani ya Klabu hiyo.

Related

michezo 9038862725056471291

Post a Comment

emo-but-icon

item