Mwigizaji nyota wa Bollywood afariki dunia .


                                     Shashi Kapoor amecheza filamu zaidi ya 50.

INDIA,Mumbai

MWIGIZAJI mkongwe wa Bollywood  Shashi Kapoor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.Kapoor, aliyeigiza katika filamu maarufu kutoka India kama vile Deewar na Kabhie Kabhie, amekuwa akiuguza kwa muda na alikuwa amelazwa hospitali.

Shashi anatoka familia ya Kapoor ambayo imetawala tasnia ya filamu za Kihindi kwa miongo mingi. Alishinda tuzo nyingi za filamu za taifa na alitunukiwa tuzo kuu ya heshima inayopewa raia na serikali ya India mwaka 2011, tuzo ya Padma Bhushan.

Ambapo Aliigiza pia katika filamu kadha za Uingereza na Marekani.Kapoor amefariki akitibiwa katika hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani mjini Mumbai.Takwimu zinaonyesha amecheza filamu zaidi ya 50.

Hata hivyo mpwa wake Randhir Kapoor ameambia Press Trust of India kwamba Kapoor amekuwa akitatizwa na figo kwa miaka mingi.

Alikuwa amemuoa mwigizaji mwingereza Jennifer Kendal, ambaye kwa pamoja walianzisha ukumbi maarufu wa sanaa Mumbai wa Prithvi mwaka 1978.



Related

burudani 3148094328449156349

Post a Comment

emo-but-icon

item