Siri ya Mkomola kutua Yanga yatajwa

Mshambuliaji wa Ngorongoro Heroes na Timu ya Taifa Yohanna Mkomola ambaye siku kadhaa zilizopita klabu ya Yanga kupitia kwa Afisa habari wake alithibitisha kuwa ni moja kati ya wachezaji wawili waliosaini Yanga Dirisha dogo yeye na Fiston siri ya kuwatosa waarabu na kujiunga na Yanga imebainika.
Moja kati ya watu wa Karibu wa Mkomola  ,amesema kilichosababisha Mkomola kuachana na Etoile Du Sahel ni masuala ya Kimkataba na siyo kitu kingine.
” Sikia nikuambie kitu, Mkomola alikuwa tayari kucheza Etoile Du Sahel lakini walishindwana kwenye masaula ya Kimkataba na Mkomola akaamua kuachana nao na Kujiunga na Yanga. ”
Mkomola anajiunga na Yanga kwa masharti ya inapotokea timu ya Nje inamwitaji kwenda kufanya Majaribio nje anaruhusiwa na Tayari kuna taarifa ambazo siyo rasmi sana kuwa mwezi ujao Mkomola ataenda Sweden kwaajili ya Majaribio ya Kucheza soka la Kulipwa.

Related

michezo 8833002040602107223

Post a Comment

emo-but-icon

item