DC Temeke azindua kamati ya ujenzi
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/dc-temeke-azindua-kamati-ya-ujenzi.html
MKUU wa Wilaya ya Temeke , Mh: Felix Lyaniva, amezindua kamati ya ujenzi wa kituo kisasa cha polisi katika kata ya Chamazi.
Katika uzinduzi huo, DC Lyaniva, amesema kuwa kuimalika kwa ujenzi wa Kituo hicho kutaimarisha ulinzi na kutokomeza vitendo vya uhalifu mbalimbali.
Hata hivyo DC Lyaniva, amewaasa na kuwatia moyo watendaji wa kamati hiyo kufanya kazi kwa weledi,uaminifu na uwazi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Ujenzi wa kituo cha polisi kata ya Chamazi unajengwa na wadau mbalimbali wa Temeke ili kutokomeza vitendo vya uhalifu na kuweka ulinzi madhubuti katika kata hiyo.