Hili ndio bifu lilotokea baada ya Chelsea na Liverpool

JUMAMOSI iliyopita tulishuhudia vigogo Chelsea na Liverpool vikitoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao moja katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliopigwa kwenye dimba la Anfield.
Baada ya mchezo huo nyota Sadio Mane alionekana kumfuata kocha wake Jurgen Klopp na kuzungumza kwa sekunde kadhaa huku wote wawili wakionekana ni wenye hisia kali katika mazungumzo hayo.
Sky Sports ilifanya mahojiano na wawili hao kutaka kujua walichokuwa wakizungumza baada ya mchezo huo ambao Klopp aliwaweka benchi Mane na Firmino.
Hiki ndicho alichosema Klopp

“Nilikuwa nampigia kelele kwavile alikuwa eneo la kati ambapo alipaswa kuwepo Mo Salah, lakini hakuna mchezaji anafurahia jambo hilo unaingia uwanjani zikiwa zimesalia dakika tatu na unajisikia kama umeshacheza dakika 150.

“Nilitaka kurekebisha hilo kwa haraka. Hakufurahia jambo hilo na akaniambia ‘Mo (Salah) ndiye alitaka tubadilishane’ lakini Mo tayari alikuwa ameshacheza takribani dakika 90,” alisema Klopp.
Sadio Mane
Mane akafunguka hivi;
“Aliponiingiza uwanjani alitaka nicheze upande wa kulia, lakini mara moja tu niliomba mpira nikiwa katika eneo la namba tisa wakati huo Mo (Salah) alikuwa upande wangu wa kulia.
“Ndipo nilipomsikia kocha akifoka ‘Sadio, njoo upande wako wa kulia’, sasa baada ya mechi nikamfuata na kumwambia ingekuwa rahisi zaidi kwake kumwambia Salah aingie katikati kuliko kunipigia kelele mimi nisogee kulia kwavile Salah ndiye alikuwa yuko jirani yake zaidi.
“Lakini ilikuwa ni kiurafiki tu, sikuongea vile kwa sababu labda nilikasirika au la, hapana. Hakukuwa na tatizo, nilikuwa najaribu tu kumweleza jambo hilo baada ya mechi.

Related

michezo 1574213500398989696

Post a Comment

emo-but-icon

item