RC Makonda afunguka baada ya mapokezi ya Ahmed Albaity

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/04/rc-makonda-afunguka-baada-ya-mapokezi.html
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amempokea Kijana Ahmed Albaity kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere mara baada ya kuwasili kwa kija huyo ambaye alisafiri kwenda Nchini China mara baada ya kusumbuliwa na tatizo la Uti wa Mgongo lililompelekea kulala kitandani kwa takribani miaka 10.
RC Makonda amefurahishwa na tabasamu alilolionyesha Kijana Albaity hii ikiashiria kwamba hali yake ya afya imeanza kuimarika taratibu mara baada ya kupatiwa matibabu.
Katika kuonesha ubinadamu kama kiongozi wa watu na mtu mwenye upendo, RC Makonda amemletea zawadi ya Ua kama ishara ya upendo kwa kijana huyo.
"Hii ni mara nyingine ya kumpokea kijana mwenzetu, ndugu yetu kipenzi kwani kurudi kwake salama kumeleta mafanikio makubwa sana ya kuona mwenzetu akirudi katika hali yake ya kawaida na furaha kubwa aliyoipoteza zaidi ya miaka 10 akiwa kitandani ni jambo la kumshukuru Mungu"amesema RC Makonda
Ahmed Albaity alifanikwa kwenda nchini China kwa ajli ya matibabu ya muda wa Wiki tatu ambapo aliambatana na wasaidizi Wawili ambapo Gharama za Matibabu zilizotumika ni zaidi ya Dola 40,000 za Marekani ambapo Sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha Dolla 27,000.
RC Makonda, alianya jitihada zote kuhakikisha Ahmed anapatiwa Matibabu ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema.
Naye Albaity amepata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutua huku akisema kwa sasa anaona unafuu tofauti na mwanzo ambapo hadi kuhisi mishipa ya damu inafanyakazi na vidole vyake vinanyambulika jambo ambalo awali alikuwa akilikosa.
"Namshukuru Mungu nimerudi tena nchini mwangu nikiwa salam, namshukuru sana Kaka Yangu, kiongozi wangu ambaye ni RC Makonda kwa jitihada zake na wale wote waliopo nyuma yangu wengine wakiniombea dua mungu awabariki kwani sasa afya yangu kidogo imetengamaa tofauti na mwanzo "amesema Albaity
Hata hivyo, katika mazungumzo na Waandishi wa habari, Albaity ameweka bayana kuhusu huduma zake huku akisema mara baada ya kufikisha miezi 6 ataanza kuona mabadiliko katika afya yake hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa afya na madaktari Bingwa wa China ambapo ndipo alipolazwa.
Ikumbukwe kwamba Alabity alilazwa nchini China kwenye Hositali ijulikanayo kwa jina la Puhua Beijing International Hospital.