Meya Kinondoni azindua Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Uzazi


MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Benjamin amefanya uzinduzi wa  utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi katika Hospitali ya Magomeni ambapo jumla ya Watoto 5562 wanatarajiwa kuchanjwa chanjo hiyo, huku watoto walio Shuleni wakifikia 4581 sawa na 82% wakati wanaotoka mtaani wanafikia 981 sawa na 18%.
Chanjo hii itachanjwa kwa watoto wenye umri wa miaka 14 kwa awamu ya kwanza, ambapo mpango wa kuwachanja mabinti wote wa kuanzia umri wa 9-14 itafanyika kwa mwaka 2019.
Uzinduzi huo uliudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo  Waalimu kutoka Shule za Msingi na Sekondari, Mratibu wa elimu na Chanjo Shuleni katika Manispaa ya Kinondoni, Mratibu wa afya Mama na Mtoto Manispaa ya Kinondoni, Mratibu wa Chanjo ya Saratani Mkoa wa Dar es Salaam , Mganga mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na  wataalam kutoka Wizara ya Afya,wataalam wa Afya kutoka Manispaa.
.
Meya Sitta, ametoa  shukrani zake kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kuleta mabadiliko katika sekta ya afya hususani afya za wakina mama.

 '' Serikali imetumia gharama kubwa kutoa chanjo hii hivyo wazazi,walezi na jamii nzima tuhakikishe wasichana wenye umri wa miaka 14 wanapata chanjo kwa awamu zote mbili bila kukosa''.amesema Meya Sitta

Katika hatua nyigine, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dr Festo John Dugange, amesema kuwa a chanjo hii itapunguza wimbi la maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi katika taifa letu hivyo wazazi wasipuuze.

Akitoa somo kwa wanafunzi hao juu ya saratani,Dr Festo Dugange, amewataka  wanafunzi wasiwe na hofu kwani chanjo hiyo ni salama na haina madhara kabisa.

Amesisitiza  kwamba Chanjo hiyo imethibitishwa kitaifa na kimataifa na imethibitishwa na shirika la afya Duniani (WHO).

"Chanjo hii ni salama na haina madhara kabisa hivyo kuwataka baada ya miezi sita kurudia chanjo ya pili ili kukamilisha dozi kamili"amesema Dr Dugange 

Naye  Mratibu wa afya Mama na Mtoto Manispaa ya Kinondoni, Bi: Edith Mboga, amepata wasaa wa  kuwausia watoto hao, namna ya kujilinda na kujichunga dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kuepuka ngono zembe,kuacha tamaa.Huku wakitolea mifano katika vitabu vitakatifu jinsi vinavyokataza kuacha anasa na dhambi.

"Pia  huduma hi itatolewa katika shule 223  za manispaa ya Kinondoni , ambapo tayari walimu 263 wamepewa mafunzo  ya uhamasishaji chanjo hiyo. Pia watumishi wa afya 66 wamepewa  mafunzo hayo,"aamesema  Editha.

 Amesema kuwa jumla ya 30% ya Wagonjwa wanaoenda katika Hospitali ya Ocean Road ni wagonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi, huku 10%  ya watoto hupata ugonjwa huo.


Chanjo hii ilizinduliwa na Makamu wa Rais kitaifa katika viwanja vya Mbaragala Rangi tatu na kwa sasa inaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika Wilaya ya TKinondoni  chanjo hii itatolewa katika vituo 292 ,ambapo vituo  29  vitatumika katika Manispaa ya Kinondoni na  vituo 263 ni katika vituo vya afya.Takribani wasichana 5562  wanatarajiwa kupata chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi.Ambao itajumuisha idadi ya wale waliopo mashuleni na nyumbani.

Related

habari 6511495687598100031

Post a Comment

emo-but-icon

item