DR Congo: Watalii wa Uingereza watekwa nyara katika mbuga ya Virunga

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/dr-congo-watalii-wa-uingereza-watekwa.html

Watalii wawili wa Uingereza ni miongoni mwa watu watatu waliotekwa nyara katika mbuga moja nchini DR Congo(DRC).
Mkurugenzi wa mbuga ya wanyama pori ya Virunga - inayojulikana kwa sokwe wake wanaosihi milimani amesema kuwa gari lao lilivamiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki ambao walimuua afisa wa kulinda wanyama pori na kumteka nyara dereva wake.
Kisa hicho kilifanyika Kaskazini mwa mji wa Goma mkoani Kaskazini mwa Kivu. Afisi ya maswala ya kigeni imesema kuwa inazisaidia familia hizo.
- Watu 26 wauawa katika shambulio Burundi
- Mama anayenyonyesha mtoto 'aaibishwa' katika mgahawa Kenya
- ''Hapana, ahsante sina haja'',Zari Hassan amjibu msanii wa Kenya
Pia imesema kuwa inawasiliana kwa karibu na mamlaka ya DR Congo. Vyombo vya habari vinasema kuwa afisa aliyepigwa risasi hadi kufa alikuwa mwanamke huku raia hao wa Uingereza wakitekwa pamoja na dereva wao raia wa Congo.
Mkurugenzi wa mbuga hiyo Emmanuel de Merode aliambia AFP kwamba: Naweza kuthibitisha kwamba gari letu lilishambuliwa. Watu watatu walitekwa nyara wakiwemo watalii wawili.
Mwandishi wa BBC Luisse Dewast, ambaye alikuwa akiripoti kutoka taifa hilo amesema kuwa hali ni mbaya sana.
Alisema kuwa kulikuwa na makundi ya watu waliojihami ambayo yalikuwa yakitekeleza operesheni zake ndani ya mbuga hiyo na kumekuwa na utekaji hapo awali ambao umehusisha ulipaji wa fidia.
Utekaji huo ulifanyika katika eneo moja la kijeshi na kwamba jeshi la taifa hilo lilikuwa likijaribu kukabiliana na hali hiyo.

Mbuga hiyo iliopo kati ya mpaka na Uganda na Rwanda ina ukubwa wa maili 3000 mraba.