Diwani Kijichi amuunga mkono Rais Maufuli kwa vitendo baada ya kufanikisha kuwasaidia Vijana wake elimu bure kuhitimu mafunzo ya Kompyuta

Diwani wa Kata ya Kijichi, Eliasa Mtarawanje, amehitimisha moja ya malengo yake ya kusomesha Vijana wake bure katika ujunzi wa Kompyuta uliosimamiwa kwa kushirikiana na DOT.
   Mhe.Diwani akitoa Cheti {Certificate{Kwa Mwanafunzi aliehitimu Mafunzo hayo.

 Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo kwenye Kata yake, Mtarawanje amewashukuru  wahisani wa DOT {Digital Opportunity Trust}kwa kumuunga mkono katika Harakati Zake za kutaka kutoa Elimu ya Kompyuta Bure katika kata hiyo. 

Baadhi ya wahitimu wa Elimu ya Compyuta.

Leo hii vijana 60 wamehitimu mafunzo hayo,ambapo ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kuunga mkono Jitihada za Rais Magufuli za kuitaka Tanzania Kuwa Nchi ya Viwanda ambapo vijana wakiipata Elimu hupelekea kurahisisha Ndoto Zake.

"Maisha ya Viwanda Lazima yawe ya Digitali,inamaana Elimu hii ya Compyuta itawapelekea wao wenyewe kujiajili kwa sababu watu hawa wa DOT wamefundisha Nyanja Mbalimbali''Amesema Mtarawanje
Aidha Mhe.Diwani amesema Vijana hao kwa sasa wameweza kujitambua katika matumizi mazuri ya Compyuta ,Huku akiwataka Vijana wengine watumie Fursa Hiyo kutokana na masomo hayo kuwa ni endelevu.
Amebainisha kuwa kuhitimu huko ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wengine wapya katika wiki inayofuata siku ya Juma tatu 14 Mwezi huu.
Wanafunzi wakionyesha vyeti vyao baada ya kuhitimu.

Katika Hatua Hiyohiyo Diwani Mtarawanje ametoa Fursa Nyingine kwa Akina Mama wajasiliamali  kupatiwa Elimu ya Ujasiliamali  hivyo amewataka kujitokeza kwa Wingi ili kupatiwa Ufahamu Mzuri wa Kujikimu Kimaisha.
Hata Hivyo Diwani Huyo amewaahidi vijana hao kuwa nao nega kwa bega ambapo amewahakikishia kuwa ataendelea kuwatafutia Fursa Nyingine.

Kwa upande wake Mmoja wa Wanafunzi hao Bi.Odda Rashid Kambangwa ,Ametoa Shukrani zake za Dhati kwa Diwani Huyo kwa kuwapigania ikiwa ni jitihada zake Binafsi za kutaka kuwaona Vijana Hao wanapiga hatua mbele kimaisha,ambapo pia ameeleza kuitumia vizuri Elimu hiyo aliyoipata katika kujipatia Kipato.
Winnie Plangyo ni Mwalimu wa Elimu ya Kompyuta ameeleza kuwa  vijana hao wameitikia vema Fursa hiyo ambapo wameweza kujitokeza kwa wingi ,na kusema kuwa wamekuwa wakimpa Ushirikiano Mkubwa wakati wa Mafunzo hayo.

Related

habari 1314582434019383652

Post a Comment

emo-but-icon

item