Katibu CCM Wilaya ya Ilala ahimiza viongozi kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala, Joyce Mkaungala , amewataka Viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya shina hadi Wilaya kuhakikisha wanachukua matatizo ya wananchi wao na kuyafanyia kazi kama ilani  ya chama inavyosema.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema  Ofisini kwake Ilala Boma ,Jijini Dar es Salaam, Joyce, amewataka Viongozi kuachana na siasa uchwara na badala yake kuwatumikia wananchi kutokana na mpangilio imara wa ilani ya chama na utekelezaji wake.
Joyce, amesema huu sio muda wa kucheza ni wakati wa watendaji kutenda kazi kwa vitendo na kuhakikisha wanachukua jitihada mbali mbali za kutatua kero za wananchi ili waendelee kujenga imani na chama hicho.
Amesema katika kuhakikisha kero za wananchi wa Wilaya ya Ilala zinatatuliwa, wapo tayari kushirikiana na Uongozi wa ngazi za juu ili kufichua uozo unaofanywa  na baadhi ya watendaji ambao si waaminifu wenye lengo la kutia doa Chama cha CCM ambacho kinadhamira ya kumkomboa mnyonge na masikini.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joyce Mkaungala, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, kulia ni Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Sultani Side 
“Sisi kama watendaji wa juu wa Wilaya tuna jukumu la kuwakumbusha watendaji wa ngazi za Kata na Serikali za mitaa kupitia CCM katika kutekeleza ilani ya Chama, hivyo tunawaomba viongozi wote wahakikishe kero zinatatuliwa, wanachukua hatua madhubuti ili watu waendelee kukiamini chama katika utendaji wake uliotukuka chini ya Rais John Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama”,amesema Joyce
Katika hatua niyingine, Joyce, amesema wapo kwenye mkakati mkubwa wa kuhakikisha wanakutana na Wenyeviti wa Mitaa wote waliochaguliwa kupitia tiketi ya CCM ili kuangalia ni kwa namna gani wataweza kusaidiana katika kufanikisha maadhimio ya Chama na Ilani zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa na kuona chanagamoto ambazo zinawakuta na kuzifanyia kazi.

Pia, amesema hawafurahishwi na kauli mbaya zinazotolewa na Upinzani huku akidai kwamba watu hao ni vibaraka wa Mabepari na  kauli za kiuchochezi zenye lengo la kumchafua Rais John Magufuli, hivyo wanalaani kwa kauli moja na kuwataka wale wenye kufanya hivyo vyombo vya usalama viwajibike kwa kiasi kikubwa katika kuwaajibisha ili nchi iwe na amani kwani kuipoteza amani kunaweza kupelekea machafuko makubwa

“Hatuwezi kuvumilia, kama hawa wanatumiwa kama vibaraka wa Mabepari, hatutasita kuchukua uamuzi mgumu, tunahitaji nchi tulivu, angalia Libya kipindi cha Gadaf na wakati huu mambo yakoje, wananyanyasika mlo mmoja kwa siku, wazee na mababa zetu na watoto wanateseka, leo hii ikitokea kwetu hata Machinga watashindwa kuweka mitumba yao sokoni , tuavipinga vitendo hivi tunahitaji watu hawa washughulikiwe “ameongeza Joyce

Naye Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ilala, Said Sultan Side, amewataka Madiwani kuwajibika kwa wananchi wao na kufanya yale waliyoyaahidi wakati wa kampeni ili kutimiza sera zao na kukitangaza vyema chama cha Mapinduzi kwa kusimamia vyema Ilani ya chama.
Amesema kwa sasa pamoja na kuwa na changamoto kadhaa, bado chama kinaendelea  kuelimisha Vijana kuhusiana na gawio la asilimia 5 kutoka Halimashauri , hivyo amewataka wahusika kulegeza masharti katika kutoa mikopo ili kila mtanzania na Kijana anufaike na keki ya Taifa kupitia Halimashauri .

Pia ametoa wito na angalizo  kuhusiana na Wenyeviti wa Mitaa kuwatoza pesa Wananchi wanapohitaji huduma kwmba tabia hiyo haikubaliki ndani ya CCM , hivyo kwa wale watakao bainika wanafanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


“Nipende kuwaomba Viongozi acheni tabia hiyo, hata kwenye kampeni Ilani ya chama chetu haikuelekeza hayo mambo, wito wangu kwa wananchi kama mtawabaini viongozi hao tuleteeni majina yao tutawashughulikia ,”amesema Sultani

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online



Related

habari 6940159200038510770

Post a Comment

emo-but-icon

item