IYF kuanza mafunzo yao wiki hii

MKURUGENZI wa Shirika linalojihusisha na Vijana hapa Tanzania IYF , Jeon Yong , amesema wapo kwenye mchakato wa kuanza mafunzo ya kujiandaa na safari kwa Vijana wa Kitanzania watakaoenda kujitolea  Ng’ambo.

Hayo ameyasema leo kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, baada ya kukutana naWanafunzi wa Chuo hicho katika kuwapatia semina za mafunzo ya elimu ya moyo.
Amesema kuwa kuanzia Ijumaa ya wiki hii, wataanza mafunzo kwa ajili ya kuwaandaa Vijana watakao jitolea kwa kazi za Ng’ambo.

“Najivunia Tanzania ni mpango ambao unalengo la kuwafanya Vijana wawe na moyo wa uzalendo katika  kutumikia watu wote, Taifa lolote linaloendelea linahitaji viongozi wazalendo, sisi kama IYF tunahakikisha Vijana wa Kitanzania na wa Mataifa mengine wananufaika na elimu ya moyo ili kuleta maendeleo kwa Taifa”, amesema Yong
Amesema, kazi za kujitolea zinalengo la kufundisha Vijana jinsi ya kufundishana elimu ya moyo kwa mataifa mbali mbali .

Aidha, amesema mpango wake kwa sasa ni kuhakikisha anakutana na Vyombo vya habari hapa nchini kwa ajili ya kuzungumza nao ili kupata wawakilishi watakao habarisha  Watanzania kujifunza tamaduni za Ng’ambo .
Hata hivyo, amesema kila nchi inamahusiano na Vyombo vya habari , huku IYF ikitambulika kwa Mataifa mbali mbali kutokana na kazi zao wanazofanya.
Amesema atahakikisha kwamba Vinaja watakao kwenda Ng’ambo wanatuma taarifa kutokana na makubaliano na vyombo husika vya habari mara mbili kwa wiki au mara moja kwa mwezi.

Naye Afisa habari wa IYF, Mwazani Ramadhani, amesema kwa sasa wapo kwenye michakato ya kuhakikisha elimu ya moyo inatolewa kwa watu wenye rika zote na shule mbali mbali.
Amesema kama Vijana watafanya kazi vizuri watailetea sifa nchi yao na kuitangaza kimataifa na kuchangia uaminifu Miongoni mwa Vijana wa Kitanzania.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

habari 8130715970490730253

Post a Comment

emo-but-icon

item