Mwenyekiti Mji Mpya aamuru soko kufunguliwa

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Justine Chiganga, ameamuru soko la mtaa huo kuwa wazi ili wananchi wafanye biashara zao.
Mwenyekiti wa Mji Mpya, Kata Ya Mabwepande, Justine Chiganga akizungumza na waanchi khusu mpango wa soko hivi karibuni 
Akizungumza na Raia Tanzania hivi karibuni , Chiganga, amesema , wananchi wanapata tabu sana ya kutafuta chakula hadi kufikia kutoka nje ya mji jambo ambalo ni kero na kikwazo kwao.
Amesema, huduma ya chakula ni haki ya msingi, hivyo kama huduma hiyo inasogezwa karibu wananchi hawatapata tabu tena ya kutembea umbali mrefu kutafuta chakula.

Hata hivyo, Chiganga, amesema eneo hilo ni muda mrefu lilikuwa tayari kutumika lakini kutokana na zuio  la Manispaa ya kutokufanya kazi , lilikuwa kikwazo kwao huku akida kwamba waliweka pingamizi hadi leo hawajatokea.

“Hili eneo tuligaiwa na Manispaa ya Kinondoni kama watu wa kundi maalumu, chakushangaza baadae tulinyang’anywa na kuambiwa lina utata kwamba kuna watu wanne ambao hawajulikani ndio wamiliki wa eneo hili”amesema Chiganga

Amesema walishafika hadi kwa mwanasheria wao wakipeleka malalamiko yao juu ya upatikanaji wa huduma za soko na kituo cha mabasi, lakini mpaka leo hawajapatiwa ufumbuzi huku wakiambiwa wasitumie eneo hilo  mpaka pale hao watu wtakapojitokeza.



Aidha, Chiganga, amewataka wananchi kufungua eneo hilo na kufanya shughuli zao kwani wao wana haki kama ilivyo kwa watu wengine.

Baadhi ya wananchi wakikagua mandhari ya eneo  la Soko la Mji Mpya ambalo limefunguliwa leo na Mwenyekiti Chiganga
Soko hilo limefunguliwa leo , huku Mwenyekiti akijaribu kupanga utaraibu wa jinsi gani wafanya biashara wanaweza kufanya shughuli zao katika kuwaletea maendeleo
Naye mkazi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema wamechoka kula aina moja ya mboga hivyo kuwepo na soko eneo hilo kutwasaidia kubadisha vyakula na watajipatia kipato kuppitia baishara zao za ujasiriamali.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online


Related

habari 7636987894782925274

Post a Comment

emo-but-icon

item