Katibu CCM Wilaya ya Ilala atoa tamko kufuatia vurugu tawi la CCM Jangwani

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/03/katibu-ccm-wilaya-ya-ilala-atoa-tamko.html
KATIBU wa CCM Wilaya ya Ilala Joyce Mkagaula, ametoa tamko kali kufuatia kitendo cha waliokuwa Viongozi wa zamani na kufukuzwa uanachama kufanya vurugu jana katika tawi la CCM mtambani Kata ya Jangwani Wilaya ya Ilala wakidai eneo hilo ni mali yao na wapo kihalali .
Katibu Joyce amewaagiza Viongozi waliokuwepo madarakani kuhakikisha watu hao hawasogei eneo hilo wala kujihusisha na masuala yoyote ya kisiasa kwa kile kianchodaiwa uhaini wa chama, kwani madai yao ya ulipaji kodi hadi 2018 hayana mashiko kwani chama nacho kinalipia kodi hiyo hiyo kama wanavyosema wao tena kwa ushahidi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kutembelea tawi hilo lilokutwa na misuko suko baada ya Viongozi wao wa ngazi za juu ikiwamo Diwani wa kata ya Jangwani, Mh: Abdully Jafari, katibu mwenezi wa kata, katibu pamoja na viongozi wengine kufikishwa Polisi, amesema kitendo hicho hakifai katika chama na kama wapo viongozi wenye malengo ya kukichafua chama baada ya kufukuzwa kwa maslahi yao binafsi chama kitawafanyia kazi mara moja.
Amesema pesa walizokula ikiwemo za fidia na malupu lupu mengine zinatosha, hivyo kama chama hawapendi kuona tukio kama hilo linajitokeza tena huku akidai ni uhujumu uchumi wa chama pamoja na ukiukwaji wa usimamizi wa mali za chama.
“Napenda kuwapa pole wale wote mliokamatwa jana, tunajua kuna watu kazi yao ni kuharibu wakiwa na lengo la kurudisha nyuma maendeleo ya chama na wananchi wake, sisi kama chama hatutakubaliana na vitendo hivyo tutakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha rasilimali za chama zinalindwa kwa manufaa ya watu wote na sio kwa mtu mmoja mmoja “,amesema Joyce
Hata hivyo, amewataka wale waajiriwa wote walioajiriwa na Serikali chini ya utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM), huku wakidai hawatambui chama hicho,sasa wanatakiwa kuheshimu miiko ya CCM huku wafikie mahala wakatambua ajira zao zipo chini ya CCM, hivyo kama wanakula mishahara ya bure hawaheshimu chama basi watakula sahani moja ili kulinda heshima ya chama kwa maslahi ya Taifa.
Aidha, Joyce, amewataka wana CCM kujenga nguvu moja na utamaduni wa kuhakikisha mali za chama zinalindwa na wao wenyewe, lakini suala hilo litawezekana endapo watachagua viongozi makini, wenye kufuata misingi bora ya kiutawala , sio kuchaguana kirafiki matokeo yake yanatokea kama yaliyotokea leo
“Kesi ipo mahakamani,na kesi hii ni ya kudharirishwa chama na watu wake, napenda kutoa angalizo kwamba, kama kuna muajiriwa yoyote wa ngazi za kiusalama awe askari au kiongozi wa serikalini wanaendelea kushirikiana na wakina Kingaru basi tunahakikisha watu hawa tunawashughurikia mara moja kwakuwa CCM ndio chama kinachoshika dola, sasa kama kuna mtu anasema hatambui chama je anakitambua chama gani kam sio CCM ?“amefafanua zaidi kwa swali
Pia, Joyce, amelaani kitendo cha viongozi waliopo kwenye mamlaka na kutumia vibaya mali za chama na kuwaita adui wa chama , lakini ameenda mbali zaidi huku akisema wale wote ambao wamekidharirisha chama ni marufuku kufika eneo hilo na endapo wataonekana basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa zidi yao.

Mbali na hapo, amewashukuru na kuwapongeza Wazee wa chama pamoja na wale wote waliojitokeza na kujitoa kwa ajili ya maslahi ya chama na kusema kuwa wametimiza ahadi za chama na kuwaita wazalendo wa kuapamban na kutunza pamoja na kulinda mali za chama.
Naye Diwani wa Kata ya Jangwani kupitia tiketi ya CCM, Abdully Faraji, amelaani kitendo cha jana kukamatwa na kuwekwa ndani kimeharibu na kuchafua heshima ya chama cha Mapinduzi bila kujali busara wala hadhi ya chama.
Amesema wavamizi hao walikuja kwa lengo la kuwatia doa huku wakitaka kujaribu kupaka rangi za Chadema lakini baada ya kuona wanashindwa waliamua kwenda kutafuta Polisi ndipo tukashikiriwa
“Sisi tunajitambua sana, wala hatukuwapiga bali tulikuwa tunajaribu kupambania mali za chama zisichukuliwe na matapeli, mimi kama diwani ni msimamizi mkuu wa Ilani ya CCM kupitia ngazi ya kata ni haki yangu kujua kinachofanyika lakini walinibeba wakaniweka ndani, msimamo wetu ni kwamba Ofisi hii ni mali yetu tutadumu nayo daima”,amesema Diwani
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kata ya CCM Jangwani, Bawaziri, ameupongeza Uongozi wa ngazi ya Wilaya ya CCM Ilala pamoja na Katibu Joyce, kwa kazi waliyoifanya ya kushiriki moja kwa moja katika tukio hilo mpaka wanahakikisha mambo yanakwenda sawa.
Amesema kwa vile kesi inayowakabiri ni ya Jinai, basi shughuli za kichama zitaendelea kama kawaida , lakini akawasisitizia wanachama na Viongozi wa gazi zote kuwa na Umoja na mshikamano jambo ambalo anaamini litakuwa na tija kwa maendeleo yao na kufanya uwazi wa kiutendaji.
“Mimi naushukuru sana Uongozi wa Wilaya, Mbunge na wengine wote walioko nyuma yetu wakati tunapambania chama, ila yote haya yanasababishwa na viongozi wenye uroho wa madaraka na wahujumu wa uchumi na wabadilifu wa mali za chama, tuwapinge na kukemea vikali ili tusiingie doa chama chetu imara na kimeshika dola lazima tuheshimu utawala uliopo pamoja na mali zake”amesema Bawaziri
Aidha, Bawaziri, amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili akitaka zifanyiwe kazi kupitia Wilaya, miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha wa kupanua Ofisi za chama kama Ofisi ya Tawi pamoja na Kata, eneo la kitega uchumi, tawi la mtambani na Mnazi Mmmoja halina ofisi hivyo ameomba wapatiwe nguvu ya kukimbizana na hivyo vitu.
Baada ya kikao hicho, tuhuma zidi ya Ally Mshale, zimeibuliwa na Mwenyekiti wa Kata , huku lawama nyingi akitupiwa kwa madai ya kutumia mali za chama bila faida na mikataba yake haionekani.
Mshale anatuhumiwa kwa makosa mengi na Tawi hilo la CCM Mtambani Kata ya Jangwani , huku wakidai eneo analokaa kwa sasa muda wake wa miaka 6 umemalizika lakini bado anaendelea kufanya biashara bila malipo yoyote na kukaidi agizo la Viongozi wa juu wa Chama.
Wameomba kwamba kama mtu huyo atashindwa kuonyesha vielelezo vyote, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Poul Makonda , kuingilia kati na kujua uhalali wa Ally Mshale na hiyo mikataba ambayo waliingia mwanzo ili kumiliki eneo hilo na kufanya biashara zake.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online