Wateja wa GSM kujishindia safari ya Disney Hong Kong

Kuelekea msimu wa sikukuu maduka ya GSM wanakuletea ofa maalum itakayowawezesha wateja wake kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong nchini China.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza ameeleza kuwa mteja akifanya manunuzi yatakayofikia kiasi cha shilingi laki moja na nusu (150,000) ataingizwa katika droo maalum itakoyomuwezesha kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong China.
"Endapo mteja wetu atafanya manunuzi ya kuanzia laki na nusu atafanikiwa kuingia katika droo maalum ambapo mwanzo mwa mwezi January atangazwa mshindi ambaye atapata fursa ya kusafiri Disney, Hong Kong, China" Alisema Farida.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa GSM Foundation Fahad Ahmad amesema kuwa GSM wataendelea kutoa ofa kwa wateja wao kupitia maduka yao mbalimbali jijini Dar es Salaam huku akisisitiza bidhaa ni bora na gharama yake ni nafuu kulingana na maisha ya mtanzania wa kawaida.

Related

habari 5909715141953094517

Post a Comment

emo-but-icon

item