Mratibu Kalongolela awataka Wananchi wasipuuze kinga ya Mabusha na Matende

HOSPITALI ya Mnazi Mmoja iliyoko Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imeendelea na mpango wa kupima magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli kutokomeza magonjwa hayo.
Akizungumza na Raia Tanzania Online , Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Manispaa ya Ilala, Martin Kalongolela , amesema lengo la zoezi hilo ni kutoa kinga kwa Wanachi juu ya magonjwa hayo ambayo yanahatari kubwa kwa Taifa.
Aidha, Kalongolela, amesema kuwa mpaka sasa wana jumla ya vituo 159 vinavyo ratibu zoezi hilo la upimaji ikiwemo,  Serikali za Mtaa, Vituo vya mama na Mtoto, Masokoni, kwenye mikusanyiko ya watu, Vituo vya mabasi ya kawaida na Mwendo kasi, pamoja na Shule za Msingi.
Kalongolela, amesema lengo la kutawanya vituo hivyo ni kuhakikisha wanawafikia wananchi wote walioko Wilaya ya Ilala ili kujikinga na maradhi hayo.
Mratibu huyo, amesema zoezi hili lisiishie kwa Wanaume peke yao bali hata wanawake linawahusu kwa kuondoa dhana ya kuwa na busha na kuweka dhana ya kupata Matende ya matiti, Matende ya miguu kwani mbu huyo hushambulia vifigo ambapo moja kwa moja huathiri sehemu za siri.

Hata hivyo, Kalongolela, ametoa wito na kuwataka Wanawake wajitokeze kwa wingi ili kujikinga na maradhi hayo ambapo kwa mawanamke ni vigumu kuonekana tofauti na mwanaume.
Inakisiwa watu Milioni 120 duniani wana maambukizi ya Matende , ambapo kati ya milioni 40 wamepata madhara makubwa kutokana na ugonjwa huo.
Anasema zipo dhana mbali mbali kuhusu ugonjwa wa Matende na Busha ambapo  baadhi a watu wanadai unasababihswa na kunywa maji ya madafu
“Dhana hizi si za kweli , matende na mabusha hayasababishwina maji ya madafu bali mbua aina ya Culex”. Amesema Kalongolela
Amewata wananchi kulala  kwenye neti safi na salama zilizowekwa dawa , huku akisema waliopata chanjo hiyo mwaka jana ni Milioni moja na laki mbili sawa na 88% hivyo kusudio la mwaka ujao ni kuwa na sehemu kubwa ya wapimaji wa chanjo hiyo.

Related

habari 4059880289244402226

Post a Comment

emo-but-icon

item