Shina la JPM la muunga mkono Rais Magufuli kwa jambo hili

Shina la wakereketwa la JPM, siku ya jana lilitembelea Hospitali ya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya usafi katika jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza na Raia Tanzania Online ,  Mratibu wa huduma Saidizi wa Hospitali hiyo Dkt. Wegesa Wambura, amesema kitendo cha Shina hilo kufanya usafi kiungwe mikono na watu wengine wenye nia ya kuhakikisaha suala la usafi linapewa kipaumbele hapa nchini.
Aidha, amesema kuwa moja ya sifa kubwa ya kila mtoa huduma  ni kuhakikisha  usafi unazingatiwa.
"Natoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali yetu, jambo mlilolifanya ni jambo zuri nasio nyie peke yenu lazima na wengine waige mfano kutoka kwenu hakika kila mmoja akisimamia vyema jambo hili Dar es Salaam yetu itakuwa safi na afya zitaboreka" Amesema Dkt. Wambura
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Shina hilo, Said Matimbwa amempongeza Rais Magufuli kwa hatua aliyoichukua ya kuweka Jiji safi kwani kampeni hiyo imekuwa na mchango mkubwa sana wa kuleta mabadiliko chanya huku akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kazi anaoifanya ya kusimamia vyema usafi ndani ya Wilaya yake.
Odacks John mlezi wa Shina hilo ametoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na kamati yake nzima kwa kutekeleza vyema adhma ya Rais Magufuli ya kufanya usafi.
"Jukumu letu kama Shina la JPM ni kumsaidia kampeni Rais Magufuli na kuhakikisha swala la usafi linakuwa ni kipaumbele kwetu , hivyo tunaiomba Serikali itengeneze njia ya kuwawezesha maafisa wa afya ili kuhakikisha Hospitali zote zinakuwa na mazingira safi". Amesema Odacksi

Related

HABARI PICHA 6341408801081902790

Post a Comment

emo-but-icon

item