DC Mjema awataka wazazi kuwajibika kulinda maadili ya watoto

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema wazazi wana jukumu kubwa la kulinda maadili ya mtoto kama watakuwa makini
Akizungumza na Mo7news Online, DC Mjema, amesema maadili ya watoto yameangamia kutokana na wazazi kutojishughulisha na watoto zao kitu kinachozidi kuchangia mmomonyoko wa maadili.

Aidha, DC Mjema amewataka wakina mama kushika njia iliyo njema katika kufanya yale mema ambayo Mwenyezi Mungu ameyataka na uacha yale ambayo yamekatazwa.
Hayo ameyasema kwenye ufunguzi wa maulidi upande wakina mama, yaliyofanyika shule ya Msingi Muhibmbili akta ya Tambaza Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapata mualiko huo wa kua mgeni rasmi.
"Wazazi kaeni na watoto zenu kurejesha maadili, kama mtoto anakosea wewe uwe wa kwanza kumuadabisha, kama sisi tukishindwa tunatengeneza kizazi sumu ambacho kitaleta matokeo hasi ndani ya Taifa eltu tunapoelekea Tanzania Mpya ya Viwanda".Amesema DC Mjema
Pia amesema ni jukumu la mzazi kujua mtoto wake anafanya nini hata kama yupo masomoni nje au ndani ya nchi anawajibu wa kujua maendeleo yake kwa ujumla ya kila siku na kufuatilia mienendo yake ili kubaini mapungufu na ubora wa watoto zao.
Amesema kuwa kama Wazazi watalibebea vyema jukumu la kuangalia Vijana wao katika upande wa maadili watatengeneza kizazi  kipya chenye maadili kitakachofuata misingi ya dini .
Hata hivyo , DC Mjema , amewataka wazazi mwakani watoe takwimu ya watoto waliowarejesha kwenye maadili mema ili kuona ni changamoto gani wanazokabiliana nazo na kuzichukulia hatua.

Related

habari 4329159833876513192

Post a Comment

emo-but-icon

item