PRST yajipanga na mikakati ya kukuza taaluma kwa watendaji wake

SHIRIKA  la Uhusiano wa Umma la Tanzania (PRST) limezinduliwa rasmi likiambatana na uzinduzi wa katiba leo Novemba 2, 2017 Jijini  Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania ikiwa ni kiashiria cha Shirika hilo kuanza utendaji wake wa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nicholaus William, amewashukuru waasisi wa Shirika hilo kwa kutambua umuhimu wa kuwa na chombo hicho kitakachoweza kuleta matokeo  chanya na ufanisi wa kitaaluma kwenye sekta ya Uhusiano wa Umma hapa nchini. 



Amesema kuwa na chombo kama hiko kitasaidia kuwakutanisha wadau kwa pamoja kuzungumzia changamoto zao na kuwaongezea ufanisi wa kazi juu ya taaluma hiyo.

Hata hivyo, Naibu katibu huyo amesema bado kuna changamoto kubwa katika taaluma ya Uhusiano wa Umma kwani wapo wachache wanaofanya vizuri huku wengi wao wakiwa hawajatambua vyema umuhimu na majukumu ya kazi hiyo.

Amesema ili taaluma hiyo ifanye vizuri ni lazima wawe na chombo imara cha kitaaluma ili kiwajengee uwezo wa kiutendaji .

"Ili taaluma hii ifikie mafanikio ni lazima PRST iwe makini na kuwe na chombo makini, kwani PR ndiyo taaluma pekee inayochangia 80% ya wana habari katika chombo cha habari". Amesema William

"Nawaomba Waajiri wote hapa nchini kuwaruhusu PR wote wawe kwenye chombo cha PRST ili kulinda  maadili ya kazi zao". Ameongeza William


Pia Mwenyekiti wa  PRST, Loth Makuza, amesema ni wakati wa PRST kuandaa  muongozo wa mafunzo mafupi kwa wana taaluma wake katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji  jambo ambalo litachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa heshima ya taaluma hiyo ambayo awali ilionekana kudharaulika.

Naye Katibu mkuu wa PRST, Makura Ndege, amewaomba wana taaluma wote wahakikishe wanalinda maadili ya kazi zao , kwani taaluma hiyo husaidia kukuza maendeleo makubwa ya Tasnia  hiyo hapa nchini.
Katibu Mkuu wa PRST Makura Ndege , wa kwanza kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Herrison Mwakyembe  (kati kati). 
Ndege, amesema ni lazima PR washirikiane na taasisi za elimu ili kujua wanafunzi wanasoma nini kinachohusiana na taaluma anayoisomea ili kutoa mikakati ya nini wakifanye baada ya kupata ujuzi huo.

"Lengo la kuunda chombo hiki ni kuungana kwa Wana taaluma wote ili kubeba heshima ya maafisa mahusiano hapa nchini, mkuu wa mahusiano anatakiwa kufanya mahusiano kwa jamii husika kwani maendeleo ya dunia yana hitaji PR" Amesema Ndege

Hata hivyo, Kaimu Meneja uhusiano wa Umma na Itifaki Benki kuu ya Tanzana (BOT) , Viky Msina, amesema ni wakati wa kupigana ili kuleta heshima ya PR hapa nchini.

 Katika ufunguzi huo wa katiba ya PRST, ilifuatana na zoezi la ugawaji vyeti kwa wale waliofanikisha na kupigana kwa hali na mali  katika uanzishwaji wa Shirika hilo ambapo kila aliyepatitiwa cheti ili tokana na mchango wake.

Miongoni mwa waliopata vyeti ni pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu, Mh : Benjamini Mkapa, Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Chuo kikuu cha matakatifu Augastino (SAU), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha SJMC cha Uandishi wa Habari, Innocent Mbungi, Joseph Mwakasika.


Related

habari 6240246745787575986

Post a Comment

emo-but-icon

item