Gigy Money amshukia Afande Sele
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/gigy-money-amshukia-afande-sele.html
Dar es Salaam. Mwanamuziki anayetamba na wimbo “Papa”, Giggy Money amerusha dongo kwa wanamuziki wa zamani akisema waache kumzungumzia katika mahojiano wanayofanya na vyombo vya habari, ikiwa ni siku moja tangu rapa mkongwe, Afande Sele amzungumzie.
Jana Jumatatu katika mahojiano na Kituo cha Redio cha East Africa, Afande Sele alizungumzia maadili katika muziki akiwataja Giggy Money na Msaga Sumu kuwa nyimbo zao zinakiuka misingi ya tamaduni za Kitanzania.
Afande Sele ambaye makazi yake yapo mkoani Morogoro alisema: “Giggy Money simjui hata kwa sura lakini namsikiaga kuwa ni dada ambaye anapenda kukaa uchi, anapenda kufanya vitu sijui vya aina gani huo ndio mmomonyoko wa maadili .”
Kauli hiyo imeonekana kumkera Giggy ambaye pia ni staa wa kupamba nyimbo za wasanii na kuamua kumtolea uvivu ingawa hakumtaja Afande Sele jina moja kwa moja.
Katika mtandao wa Instagram ameandika: “Wasanii wa zamani naomba mnipumzishe midomoni mwenu, maana kila interview zenu mnanitaja taja mnikome kabisa. Mnadhani mkiniongelea mimi interview zenu zitamfikia Trump Marekani? Mnikome akili zangu sio nzuri nitawaharibia, wengine badala wakate nywele zao eti wanatoa ushauri. Pelekeni bangi zenu maskani uko.”