Okwi kutua na mkewe Dar
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/okwi-kutua-na-mkewe-dar.html
MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, hivi sasa yupo Uganda na atakaporejea tu kuungana na wenzake, basi atatua na familia yake.
Okwi aliondoka nchini wiki iliyopita baada ya wachezaji wa timu hiyo kupewa mapumziko mafupi ambapo wakati anaondoka alikuwa akisumbuliwa kifundo cha mguu.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Okwi alisema yupo kwao Uganda lakini bado anaendelea na matibabu ya kifundo cha mguu ambapo atakapopona, atarejea nchini akiwa na familia yake.
“Nipo huku naendelea na matibabu yangu ya kifundo cha mguu baada ya kuumia hivi karibuni na kunifanya nikose baadhi ya michezo ya ligi kuu.
“Niliondoka huko baada ya wachezaji wote kupewa mapumziko, lakini nimepanga nikirejea basi nitakuja na familia yangu ambayo awali niliiacha huku Uganda kwa sababu hivi sasa nataka niwe nayo karibu,” alisema Okwi ambaye ana mke na watoto wawili.