Pamba kupewa kipaumbele Tanzania ya Viwanda

WAFUNGWA walioko katika magereza mbalimbali katika mkoa wa Mara, watajifunza kilimo cha zao la pamba wakikwa gerezani hili wamalizapo kifungo chao wawe waelimishaji kwa wananchwalioko katika maeneo yao kuhusu kilimo hicho, jambo ambalo litasaidia viwanda vya zao hilo kupata mali ghafi ya kutosha.

Hayo yalielezwa jana na mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima, wakati akizindua shamba darasa la zao la pamba la mkoa wa huo lilikoko katika enao la Kisangwa wilayani Bunda.

Malima alisema kuwakilimo cha zao la pamba, lazima kindelezwe ili kuinua uchumi wa mkoa huo na nchi kwa ujumla na hivyo hata wafungwa walioko gerezani lazima wafundishwe kilimo cha zao hilo ili wamalizapo vifungo vyao wakawe mabalozi wa kilimo cha zao la pamba katika jamii inayowazunguka.

Aidha, alisisitiza wananchi kulima zao hilo la pamba ili viwanda vyetu viweze kuapata mali ghafi ya kutosha na kwamba pia wananchiwalime mazao mbalimbali ya chakula ili kukabiliana na upungufu wa chakula.

Hata hivyo Malima alisema kuwa gereza la Mkoa wa Mara, tayari limekwishatenga jumla ya ekari 300 kwa ajili ya kiimo cha zao hilo wakishirikiana na halmashauri ya wilaya ya Butiama.

“Hili shamba tunataka liwela mfano kweli kweli….JKT pia wamekubali kuingia kwenye kilimo hiki cha pamba, lakinipiawakulima wadogowadogo na na nyinyi pia muendelee kulima kilimo cha zao hili. Lakini pia taasisi mbalimbali nazo zilime zao hili, tunataka mkoa wa Mara uwe namba moja katika kilimo cha zao la pamba” alisema Malima.

 











Baadhi ya wananchi walipongeza mpango na hatua hiyo ya serikali mkoani hapa kwa kuhamasisha kilimo cha zao la pamba, ikiwa ni pamoja na kuwepo mashamba darasa, ambapo sasa watalima kilimo chenye tija zaidi hali itakayowasaidiakujiinua kiuchumi.












“Mimi kama mkulima kwa kweli nimefurahishwa sana na mpango huu wa serikali yetu, zamani tulikuwa tunalima kiholelahleholela tu kwa kutupa mbegu sasa elimuhii itatusaidia sana” alisema Nestory Madulum mkulima wa kijiji cha Kisangwa.

Akitambulisha mpango huo wa shamba darasa afisa kilimo wa mkoa wa Mara, Denis Nyakisinda alisema kuwa huu mpango wa shamba darasa ameuleta mkuu wa mkoa huo, Adamu Malima, ili zao  hio liwe kubwa na la kibiashara katika Mkoa huo.
Image result for picha ya zao la pamba 

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adamu  alisema iwapo wakulima mkoani humo wakizingatia kiimo hicho watazalisha tani laki moja za zao la pamba, ambapo kwa kufuata kilimo chenye tija kila ekari moja ina uwezo wa kuzalisha kilo 800 hadi 1000, ambapo kwa sasa wakulima wanazalisha kilo 300 mpaka 400 kwa kila ekari moja.

Related

habari 408508269883359596

Post a Comment

emo-but-icon

item