Maajabu ya Bamia kiafya
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/maajabu-ya-bamia-kiafya.html
BAMIA sio neno geni kwa mtu yeyote ambaye amewahi
kutumia mboga ya aina yeyote ile hii ni aina ya kitoweo au tunda kama
watalaamu wengi wanavyoliita ambalo huapatikana sehemu zote za nchi na hupendwa
kutumiwa na wengi.
Kwa mujibu wa mtaalamu na mkufunzi wa chuo cha Tiba
na Uguzi IMTU kilichopo jijini Dar es salaam ambaye pia anahusika na kitengo
cha Afya na jamii chuoni hapo Dk Daniel Mtango alisema bamia ina vitamini A na
B ambavyo hivi humfanya mtu macho yake yaimarike zaidi na protini ambayo
hupatikana katika tunda hili ni nyingi ukilinganisha na lishe nyingine.
Mtaalamu huyo aliendelea kusema kuwa matumizi ya
bamia huwaokoa watoto na tatizo la utapiamlo,huwasaidia wale wenye matatizo ya
kisukari pia huongeza kinga za mwili ikiwemo kufanya mwili uweze kupambana na
magonjwa mbalimbali na hii inawafaa sana watu waliotharika na virusi vya
ukimwi.huwasidia katika lishe kamili ukizingatia inaimarisha kinga za mwili.
Maji yanayopatikana kwenye bamia ni mengi na ni
rafiki kwa afya ,huzuia magonjwa ya moyo
vilevile huwasaidia watoto wadogo wasipasuke uti wa mgongo na huwasaidia mama wajawazito hasa mtoto
aliyeko tumboni afya yake huimarika zaidi hata baada ya kujifungua,
Bamia ni tiba kwa watu wenye matatizo ya kuchoka
choka zaidi na wale watu ambao wana
msongo wa mawazo wanashauriwa kutumia tunda hili kwani hili huleta matokeo ya
haraka na kufanya afya zao kuimarika zaidi ikiwemo kujisikia wenye amani na
furaha muda wote unapotumia mboga hii ya bei nafuu.
Vile vile hutibu vidonda vya tumbo na kuthibiti
baceria wanaosababisha matatizo hayo,pamoja na hayo hupunguza uwezekano wa
kupata saratani,huongeza kiwango cha uzalishaji damu kwa wingi
mwilini,huimarisha nywele na kuzifanya zionekane na muonekano mzuri pamoja na
kufanya utumbo mpana ubaki katika ulaini wake na kukukinga na saratani ya
utumbo mpana.
Matumizi yake unaweza kutumia kwa kuchanganya na
kitu chochote ikiwemo uji,mchuzi,ubwabwa na vyakula vingine vingi.hata hivyo Dk
Mtango alishauri watu watumie bamia kwa wingi na kusema kwa siku unatakiwa
kutumia kikombe kimoja cha chai ambayo ni sawa na gramu mia moja zikiwa
zimekatwa katwa mbichi au zikiwa zimepikwa kwa watoto wadogo inashauriwa utumie
zilizopikwa.
Ushauri ulitolewa pia kwa wakulima walipende zao
hili na kulima kwa wingi kwani ni zao linalokuwa kwa muda mfupi na huvumilia
hali zote za hali ya hewa na uhifadhi wake ni mrahisi hata ukilikausha na jua
unaweza kuhifadhi na kulitumia muda wowote na inasemekana linapokaushwa kiwango
cha protini huongezeka mara dufu.