Dagaa mboga bei chee inayotibu magonjwa hatari duniani.


KUMEKUWA na dhana katika jamii kuwa dagaa ni kitoweo au mboga ya watu masikini. Bahati mbaya sana ni kwamba wengi wao hawana uwelewa tiba ya mboga hiyo, yumkini ndio sababu ya kuwapo kwa dhana hiyo.

Dagaa ni kitoweo kinachopatikana kwa urahisi kwa jamii nyingi hapa nchini  kutokana na uwingi wa kitoweo hicho sokoni, vibanda vya biashara ndogondogo maarufu kama magenge na sasa kutokana na kukua kwa biashara pia huuzwa kwenye maduka makubwa ya biashara (super markets).
Watalaamu wa afya na lishe wanasema dagaa ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu bila kujali kipato kutokana na faida zake mwilini, ambazo wanabainisha kuwa ni pamoja na kuzuia shambulio la moyo.
Image result for picha ya dagaa

Hiyo ni kwasababu ya kuwapo kwa virutubisho vingi  kwenye  dagaa kama vile kiwango kikubwa  cha kirutubisho aina ya Omega-3 (Fatty Acid) kilichomo .
Mmoja wa watafiti hao,  Dk. Edward Group wa nchini Marekani anaandika makala ya matokeo ya utafiti kuhusu kitoweo hicho kuwa  kutokana pia na kiasi kingi cha madini ya kalishiam yaliyomo kwenye dagaa husaidia kuimarisha mifupa mwilini.

Dk. Group ambaye pia  ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Global Healing cha nchini humo anasema katika makala yake hiyo kuwa dagaa wana vitamin D ambayo huwa nadra sana kupatikana kwenye lishe ya kawaida.

Vitamin D pia huimarisha afya ya mifupa ikisaidiana na madini ya fosforas yaliyomo kwenye dagaa, alisema.
Zaidi,  dagaa ni chanzo kizuri cha Vitamin B12 baada ya maini ambayo ndio chanzo kikuu cha vitamin hivyo.

Vitamini B12 hufanya kazi kubwa ya kuboresha ustawi wa moyo na hivyo kuwa chakula kizuri cha kumpa ahueni mgonjwa husika au kinga madhubuti mlaji dhidi ya magonjwa ya moyo.
Watafiti wengine nchini humo pia walibaini  kuwa miongoni mwa vidhibiti vya magonjwa ya saratani ni pamoja na dagaa kutokana na kuwa na kiasi kingi  cha madini ya  kalisiam ambayo husaidia kupambana na  seli zinazosambaza saratani mwilini.
Wanasema dagaa zina kiasi kingi cha protini, hudhibiti upungufu wa protini mwilini, ilisema sehemu ya makala.

Image result for picha ya dagaa
Protini husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa chembe hai mwilini na uimarishaji wa mfumo wa kinga ya mwili (body immune system) na kujenga mwili.
“Licha ya kuwa dagaa wana faida katika mwili wakati wa ulaji lakini pia ni watamu mdomoni na huleta hamu ya kula na kukufanya ule chakula kingi na kushiba,”anasema Dk. Group.


Katika tafiti nyingi za magonjwa ya moyo na tiba zake, virutubisho vya Omega 3 vimeonekana kuwa dawa au kinga muhimu ya magonjwa ya moyo ambayo yamekuwa yakitumia mamilioni ya pesa katika tiba. Tumekuwa tukishuhudia wagonjwa wengi hapa nchini wakisafirishwa nje ya nchi hasa huko Apollo nchini India kwa matibabu. Inaelezwa kuwa  chanzo kikuu cha  virutubisho hivyo ni viumbe wa majini ikiwamo samaki na dagaa.

Related

AFYA 7169586750977756610

Post a Comment

emo-but-icon

item