Asilimia 67 ya uvimbe bila maumivu ni dalili za saratani
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/asilimia-67-ya-uvimbe-bila-maumivu-ni.html
TAFITI
zinaeleza kuwa zipo baadhi ya dalili zinazojitokeza katika mwili wa binadamu
ambazo katika hali isiyo ya kawaida ni ishara kuwa mwili huo una shida na
unahitaji uchunguzi kugundua ni tatizo la aina gani.
Baadhi
ya dalili hizo zilizoelezwa na tafiti hasa kwa watoto wadogo zinazoashiria
kupatwa na ugonjwa wa saratani ni kuvimba sehemu ya mwili bila maumivu
yoyote hasa sehemu za shingo, miguu, shavu na tumboni.
Akizungumza
na Raia Tanzania mapema wiki hii, Katibu wa
Shirikisho la Vyama vya Waganga wa Tiba Asili
na Tiba Mbadala (SHIVYATIATA), lenye
makao yake Tabaa Relini Jijini Dar es Salaam Dk. Othuman Shem alisema baadhi ya
dalili katika mwili wa binadamu ni
ishara ya ugonjwa wa saratani ingawa kundi kubwa la watu halina ufahamu huo.
Dk.
Shem ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha dawa za asili cha Paseko Natural Clinic alisema utafiti uliofanywa na kampuni ya Paseko T.O
& P. Co. Ltd kwa kushirikiana na Ubalozi
wa Ireland hapa nchini, ulionesha kuwapo kwa kundi kubwa la watu
katika hamii hasa watoto kuwa na dalili hizo bila kujua kuwa ni dalili za
saratani hasa watoto.
Picha ya mtoto mwenye uvimbe. |
“Katika hatua ya kuangalia dalili hizo kwa
kushirikiana na ubalozi wa Ireland hapa nchini, tumegundua kuwa zaidi ya
asilimia 67 ya dalili hizi inaonesha kuwa huu ni ugonjwa wa saratani lakini
wengi hawajui.”alisema Dk. Shem.
Aliendelea
kusema kuwa,d alili zingine ni pamoja na mtoto wa jicho kuwa na rangi nyekundu, makengeza na
hata upofu wa ghafla.
“Pia
damu kutoka kwenye fizi, kuvia katika macho, kutapika wakati wa asubuhi, kuumwa
na kichwa kupitiliza, kukonda bila
sababu, kupungua uzito, homa inayojirudia rudia bila kuwa na chanzo, nguvu ya
mwili kupungua kuliko kawaida” alisema. Othuman.
Zaidi
ya dalili hizo, nyingine ni mtoto kupungua damu mwilini mara kwa mara, alisema
na kuongeza: “Tunaendelea kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuokoa Watanzania, hii ni pamoja na kutoa elimu hasa
vijijini ambako wengi wanakuwa na dalili hizi lakini hawazijui na kujikuta
wakipoteza maisha ama watoto au wapendwa wao,”aliongeza.