Rais Mugabe Ajiuzuru
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/rais-mugabe-ajiudhuru.html
SPIKA
wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Kwa
mujibu wa shirika la habari la Reuters limemnukuu Jacob Mudenda hatua hiyo ni
ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko ya amani.
Tangazo
hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo
zilikuwa zimeanza dhidi yake huku Spika wa bunge akisema kiongozi mpya atawekwa
madarakani siku ya Jumatano.
Wabunge
walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Mugabe
ambaye ameingia madarakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980 alikuwa
amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa
na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka madalakani wiki hii.
Mugabe
ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15
iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake huku sababu
za kumtaka ang’atuke zikiwa ni baada ya kumfuta kazi makamu wake wa rais
Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.
Hatua
hiyo ilionekana na wengi kama njama ya kumrithisha mkewe na kusababisha viongozi
wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizini.
Waziri
mkuu wa Uingereza Theresa May amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia
Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala wa
kiongozi huyo.
Amesema
kuwa Uingereza ambaye ni rafiki wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo
kusaidia kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki na kujenga uchumi wa
Zimbabwe.
Ubalozi
wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya kihistoria na kuwapongeza
raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao kwakile kilichodaiwa kuwa ni wakati wa
mabadiliko.
Kwa
mujibu wa Mwanaharakati wa haki za Binadamu Linda Masarira akiongea na BBC ninafuraha
sana leo kwa sababu nimekuwa nikiamini kwamba Mugabe atajiuzulu katika maisha
yangu.
Chama
cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance kilifurahia hatua
hiyo kikisema kuwa Mugabe alibadilika kutoka kuwa mkombozi hadi dikteta.
''Na
sasa kwenda mbele ni wakati wa upinzani kujiandaa na kuona kwamba tunakuwa na
serikali inayowajali raia wake.Na kila mtu lazima ashirikishwe''.