Meya Mwita asema mkutano wa COP 23, utatoa suluhisho la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa  mkutano wa COP 23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji mbalimbali duniani utatoa  suluhisho la pamoja la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.

Akiwa Nchini Ujerumani , Meya Mwita emesema kuwa mkutano huo  utakuwa mahususi kwa jiji la Dar es asalaam kupata suluhisho na kuhakikisha kuwa wanakabiliana  ipasavyo na mabadiliko  ya tabia ya nchi ikiwemo janga la mafuriko ambalo limekuwa ni tatizo sugu jijini hapa.
Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23  wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, COP 23  inahusu miji na Taasisi zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko hayo inayofadhiliwa na Nchi hiyo.
Mkutano huo  wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi umeandaliwa na Taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo  umeanza jana alasiri mjini Bonn nchini  Ujerumani.
Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni Jiji la  Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. 
  
Hata hivyo mkutano huo utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu ambapo    jiji la Dar es Salaam linashiriki katika likiwa na ujumbe wake unao ongozwa na Mstahiki Meya Jiji hilo  Mwita pamoja na  Mkurugenzi  Sipora Liana.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

SIASA 8243853208071126275

Post a Comment

  1. Gazeti makini kwa watu makini , hapa tunapata taarifa muhimu

    ReplyDelete

emo-but-icon

item