Rais Magufuli aweka rasmi jiwe la ujenzi wa bomba la mafuta Uganda
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/rais-magufuli-aweka-rasmi-jiwe-la.html
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikanamkono na
kupongezana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada
ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima
nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga. Sherehe za uwekaji wa jiwe
hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani Kyotera nchini Uganda
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya bomba hilo la
mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa maelezo ya mradi
huo mkubwa wa bomba la mafuta ghafi.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula mara baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni
katika eneo la mpaka wa Tanzania Mutukula kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja
cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania na Uganda.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais
wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili upande wa Tanzania
kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa
Tanzania na Uganda.
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni
wakiangalia ngoma katika eneo la Mutukula upande wa Uganda.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama
Janeth Magufuli wakifurahia ngoma za asili za
watoto wa Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo huku Rais wa Uganda
Yoweri Musevini akitazama watoto hao.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais
wa Uganda Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za mataifa ya Tanzania na Uganda
zikipigwa katika eneo la Uganda.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Uganda Yoweri
Museveni wakifungua Ofisi za Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande
wa Tanzania. Wanne kutoka kushoto ni Mke wa
wa Rais Mama Janeth Magufuli akishuhudia pamoja na Mke wa Rais Museveni
Mama Janeth Museveni wa kwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda
Yoweri Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika
eneo la Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta. PICHA
NA IKULU
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online