Wakazi wa kitongoji cha Mbugani wakabiliwa na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara

WAKAZI wa kitongoji cha Mbugani katika halmashauri ya mji wa Bunda, mkoani Mara, wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara pamoja na madaraja katika eneo hilo, hali ambayo uhatarisha maisha yao, wakiwemo wanafunzi wanaokwenda au kutoka shuleni.
Image result for Wakazi wa kitongoji cha Mbugani

Wananchi wa kitongoji hicho jana walimwambia mkuu wa wilaya ya Bunda, aliyetembelea eneo hilo, kuwa changamoto hiyo ni ya muda mrefu, licha ya kuwaambia viongozi wao akiwemo diwani wa kata hiyo, lakini bado haijapatiwa ufumbuzi wowote na wanendelea kutaabika kwani hakuna barabara hata madaraja ya uhakika.

Walisema kuwa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja katika eneo hilo siyo rafiki kwa maisha yao, hususani pindi mvua zinaponyesha, kwani barabara ukatika na kusababisha mafuriko makubwa na maji kujaa hadi kwenye makazi yao.

Walisema kuwa hali hiyo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na idara ya ardhi katika halmashauri hiyo kugawa viwanja kiholela bila mpangilio maalumu hadi kwenye maeneo ambayo siyo rasimi, ambapo husababisha maji kukosa mwelekeo na kuingia kwenye nyumba zao.

“Mkuu wa Wilaya hali hii imesababishwa na iadara ya ardhi kugawa viwanja katika maeneo ambayo siyo rasmi na kusababisha maji kukosa mwelekeo na kuingia kwenye makazi yetu” alisema mwananchi mmoja mkazi wa eneo hilo.

Kufuatia hali hiyo wananchi hao waliiomba halmashauri ya Mji huo na serikali kwa ujumla kuwarekebishia miundombinu hiyo, ili iweze kupitika hali ambayo itawawezesha kuzifikia huduma za kijamii kwa urahisi zaidi, ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kufanya kazi za maendeleo yao pamoja na serikali kwa ujumla.

Hali hiyo ilimsukuma mkuu wa wilaya hiyo, Lydia Bupilipili, kutembelea kitongoji hicho na kujionea hali halisi ya kero hiyo, huku akishuhudia madaraja ambayo yametengenezwa kwa miti ambayo yanahatarisha maisha ya wananchi wanaovuka kwenda upende wa pili kwa kutumia madaraja hayo.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya ya Bunda Bupilipili, alisema kuwa idara ya ardhi katika halmashauri ya Mji huo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali, ikiwemo hiyo ya uharibifu wa miundombinu kutokana na ugawaji hovyo wa viwanja.

Akitoa ufafanuzi juu ya miundombinu hiyo ya barabara na madaraja, mwakilishi wa mkurugenzi wa Mji huo, ambaye ni mtumishi kutoka idara ya ujenzi, Ryoba Saranga, alisema kuwa kwa sasa hivi wanaoshughulikia kutengeneza miundombinu hiyo ni wakala wa barabara (Tarura) na kwamba watawasiliana nao ili waweze kuiondoa kero hiyo.

Na katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ya Bunda alimshukia diwani wa kata hiyo Georgs Miyawa (Chadema) kwamba amekuwa hafanyi mikutano na kuchukuwa kero za wananchi na kuzipeleka kwenye vikao husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na kwamba pia hana ushirikiano mzuri na serikali, kwa madai kuwa amekuwa akipinga kila jambo yakiwemo maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo diwani huyo aliyekuwa katika eneo hilo alikanusha vikali tuhuma ya kupinga maendeleo na kuongeza kuwa mara kwa mara amekuwa akifanya vikao na kuchukuwa kero za wananchi na kuzipeleka panapohusika.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

SIASA 195371210182937785

Post a Comment

emo-but-icon

item