Mambo 7 usiyoyajua kuhusu winga wa Man City, Leroy Sane haya hapa
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/mambo-7-usiyoyajua-kuhusu-winga-wa-man.html
7. Sehemu ambayo anakubali kuwa dhaifu anapocheza mpira.
Imezoeleka kwa wachezaji wengi kujiona wamekamilika kwa kila kitu wakiwa kiwanja lakini, kwa Lory Sane imekuwa tofauti kwani, anakubali kuwa sehemu ambayo mpaka sasa anaona ni dhaifu kwa upande wake ni Matumizi ya Mguu wa Kulia awapo kiwajani, siku zote yeye ni mzuri kwenye matumizi ya mguu wa kushoto.
6. Sane anatoka katika familia ya Michezo.
Mama yake ni Regina Weber Sane, ni mjerumani pekee (kwa upande wa wanawake) kushinda medali katika mashindano ya Olimpki katika masula ya Jim.
Baba yake ni Suleiman Sane ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Senegal, Pia alikuwa akiutumia vizuri mguu wa kushoto.
5. Leroy Sane anasherehekea siku ya kuzalia sawa na mchezaji wa Leicester City, Jamie Vardy, na Emile Heskey mchezaji wa zamani wa Liverpool.
Sane alizaliwa tarehe 11 January 1996.
4. Chakula anachokipenda ni Penne Carbonara.
Asili ya chakula hiki ni nchini Italia. Wakati anajiunga na Manchester City, Sane aliambiwa aache kunywa kinywaji cha Co cacola kwa wingi kwani alikuwa akinywa kiwango cha lita mbili kwa siku.
3. Hajawahi kushinda chochote kwenye ngazi ya Vilabu Au mchezaji binafsi.
Licha ya kucheza katika klabu kubwa ya Schalke 04 ya ujerumani na kwa sasa anakipiga katika klabu ya Manchester City bado hajapata kuchukua ubingwa huku matumaini makubwa yakiwa katika msimu huu wa 2017/2018 kwa klabu yake ya Manchester City huenda ikashinda ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza EPL kwani timu yake inaongoza kwa alama 31 huku inayofuata ( Manchester United ikiwana alama 23, kwahiyo ni tofauti ya alama 8.
2. Kitu anachokipenda zaidi ni “Mpira”
Siku zote yeye anachokiwaza ni mpira na siyo kitu kingine chochote.
- Alipata jina lake kwa heshima ya kocha wa baba yake anayejulikana kwa jina la Claude Le Roy.
Kocha huyo mwenye asili ya ufaransa alizaliwa mwaka 1948, amewahi kuzifundisha timu za taifa la Senegal, Ghana na kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.