UTATA MWINGINE WAZUKA KWENYE KLABU YAYANGA BAADA YA HAYA KUTOKEA JUU YA HAYA HAPA

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Yanga limetangaza msimamo mkali unaoweza kumuweka kwenye wakati mgumu mshambuliaji mpya wa kigeni, ambaye timu hiyo ipo mbioni kumsajili katika siku 18 zilizobakia kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa.
Msimamo uliotangazwa na benchi la ufundi la Yanga ni kuwa na imani kubwa na uwezo wa nyota wake waliopo kikosini kwa sasa huku likifichua mkakati wa kuendelea kuwapa kipaumbele na nafasi ya kucheza zaidi badala ya kuweka matumaini kwa mshambuliaji  mpya atakayesajiliwa.

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema haoni haja kwa Yanga kusajili mshambuliaji mpya kwa kipindi hiki kwa sababu waliopo wanatosheleza na wanaweza kuifanya vizuri kazi ya kupachika mabao iwapo watapewa muda mfupi wa kuimarika.

"Sidhani kama kuna haja ya kufanya usajili wa kumsajili mshambuliaji kwenye kipindi hiki kwa sababu tunaamini waliopo wanaweza kutupatia kile tunachokihitaji iwapo watakaa sawa. Kikubwa kinachohitajika kwa sasa ni washambuliaji wetu kuwa kwenye muendelezo mzuri wa ubora.

"Ukiangalia kikubwa tunachokikosa ni hicho kwamba mechi hii tunafunga mabao na nyingine tunashindwa kutumia nafasi tunazozitengeza.

"Jukumu letu kama benchi la ufundi ni kulirekebisha tatizo hilo na naamini inawezekana. Tunao washambuliaji wenye uwezo mkubwa ambao wanaweza kutupatia matokeo, Ni kuwapa nafasi ya kuimarika na nina imani tatizo la kukosa mabao litakwisha," alisema Nsajigwa.

Hata hivyo, wakati benchi la ufundi la Yanga likitoa msimamo huo wa kuweka imani kwa nyota waliopo kikosini, kamati ya usajili ya Yanga ipo msituni kusaka mshambuliaji wa kati mwenye uwezo wa hali ya juu wa kupachika mabao ikionekana kutoridhishwa na ufanisi wa waliopo.

Uongozi wa Yanga unataka kusajili mshambuliaji ambaye atawapa uhakika wa kuwa na wastani mzuri wa kufunga kulingana na nafasi anazozipata mbele ya lango la timu pinzani na kuwapunguzia mzigo Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu ambao kiasili sio washambuliaji wa kati.

Hatua hiyo ya Yanga kuingia msituni kusaka mshambuliaji wa kigeni imechochewa zaidi na kuwakosa Amissi Tambwe, majeruhi wa muda mrefu pamoja na Donald Ngoma, ambaye kwa sasa hayupo kikosini akidaiwa kuwa na mgogoro na uongozi.

Hata hivyo, Yanga kama itasajili mchezaji wa kigeni, itapaswa kumuondoa mchezaji mmoja kwani hadi sasa imetimiza idadi ya wachezaji saba kutoka nje ya nchi baada ya hivi karibuni kukamilisha usajili wa beki Fiston Kayembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mchezaji mwingine ambaye Yanga tayari wameshakamilisha usajili wake ni mshambuliaji chipukizi Yohana Nkomola, ambaye anachezea timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.kuona wachezaji waliyofukuzwa 

Related

michezo 1473770720933085353

Post a Comment

emo-but-icon

item