Himid Mao aitabiria makubwa Azam FC


WAKATI  ilionekana kama Azam FC ilikuwa inajenga timu ya wachezaji vijana hadi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, sasa mambo yamebadilika na matumaini yamekuwa ni ubingwa.Image result for HIMID MAO

Awali uongozi wa Azam FC kupitia msemaji wake Jaffar Iddi, ulisema umeshangazwa na mwendo mzuri wa vijana wao na unaweza kuwania ubingwa.

Lakini safari hii, nahodha wake Himid Mao, amesema ana matumaini makubwa ya timu yao kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Himid maarufu kama Ninja amesema baada ya timu yake kuitwanga Ruvu Shooting kwa bao 1-0 na kufikisha pointi 19.

Pointi 19 zinaifanya Azam FC kushika nafasi ya pili ikifukuzana na vinara wa ligi hiyo Simba wenye pointi kama hizo.

Simba wanasimama kileleni kutokana na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

“Msimu huu wa ligi kuu tutajitahidi kupambana kuchukua ubingwa wa ligi kuu licha ya upinzani kuongezeka kutokana na kila timu kujiandaa kuhakikisha inapata pointi tatu.

“Kama ulivyoona mwenyewe mechi yetu hii na Ruvu ilikuwa na ushindani kwa kila upande, utaona kila timu ilicheza vizuri kwa maana ya kushambulia kwa lengo la kupata pointi tatu.


“Lakini tunashukuru tukafanikiwa kupata bao dakika ya 90 ya mchezo huo na kukaa kileleni katika msimamo wa ligi kuu,” alisema Mao.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

michezo 7589499707554408045

Post a Comment

emo-but-icon

item