Ajibu aichongea Simba

WAKATI Simba ikiendelea kufurahia kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya juzi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, mshambulliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema timu yake hiyo ya zamani haina muda mrefu kukaa katika nafasi hiyo kabla hawajaikamata.
Image result for ajibu
Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa kama ilivyo kwa Simba na Singida United, Jumamosi ililazimishwa sare tasa katika Uwanja wa Namfua na wenyeji wao, Singida.

Matokeo hayo yaliifanya Yanga kufikisha pointi 17 kabla ya Jumapili Simba kurejea kileleni baada ya kuichapa Mbeya City, hivyo kufikisha pointi 19 sawa na Azam FC iliyoshinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi usiku.

Aidha, Ajibu aamesema pointi mbili walizopishana na Simba si nyingi na haziwaumizi kichwa.

Amesema ligi bado ni mbichi na hivyo mashabiki wao hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kufanya vibaya.

"Mimi ninauhakika, tunaweza kufanya vizuri, hatukutegemea kupata sare kwenye mchezo dhidi ya Singida United, lakini ndio mpira, mashabiki hawapaswi kuwa na hofu, ligi bado sana na waliopo kileleni tuna uwezo wa kuwakamata," alisema Ajibu.

Amesema  hakuna timu ambayo tayari imejihakikishia ushindi katika michezo iliyobakia ya mzunguko wa kwanza.

Katika hatua nyingine, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, aliliambia Nipashe jana kuwa, leo wanaendelea na programu yao ya mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata'

"Tumerudi jana (juzi), leo (jana) wachezaji wanapumzika na kesho tunaendelea na programu yetu ya mazoezi kwa wale ambao hawapo kwenye timu ya taifa," alisema Hafidh


Yanga mechi ijayo itasafiri kwenda kuivaa Mbeya City Jumapili Novemba 19, mwaka huu.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

michezo 8145122769519037234

Post a Comment

emo-but-icon

item