Mkurugenzi wa kituo cha Uwekezaji (TIC) amewataka DC na RC wote wakishirkiana na Taasisi mbali mbali kuandaa mazingira ya kuwavutia Wawekezaji

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/mkurugenzi-wa-kituo-cha-uwekezaji-tic.html
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Godfrey Mwambe amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja na Taasisi mbalimbali za kiserikali kufanya tathmini mara kwa mara katika maeneo ili kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kuvutia wawekezeji wengi zaidi.

Mapema leo hii akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi huyo, amesema kuwa, endapo wakuu hao wa mikoa wataweza kutenga maeneo na kufanya tathmini ya mara kwa mara wateza kupata wawekezaji wengi zaidi.
Aidha amesema,Tanzania hadi kufikia mwaka 2017 ilikua inashika nafasi ya 7 kati ya nchi 10 za Afrika zenye ushawishi wa kuvutia wawekezeji kuweza kuwekeza ambapo amesema matokeo hayo yametokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano Dkt,John Magufuli.
"Serikali ya awamu ya tano imekua ikifanya juhudi hizi kwa nguvu na msisitizo mkubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, ambayo imelekea kukuza uwekezaji nchini na kuibua fursa kubwa za ajira kwa vijana."amesema Mwambe.
Amesema kuwa, Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali zitaweka jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kutasaidia kupanua wigo wa walipa kodi, na hatimaye kuongeza uzalishaji na kufikia uchumi wa kati.
Aidha amezitaka taasisi zote nchini pamoja na mamlaka zote husika kukuza ushirikiano na kituo hicho cha uwekezaji kuweza kujenga huelewa na kutoa miongozo ili kuweza kusimamia ujenzi wa viwanda nchini.
Aliongeza kuwa, katika kuhakikisha wanaboresha uwekezaji nchini kituo hicho kimeongeza ofisi nne mpya za kanda katika mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Mtwara na kigoma ambazo ni kanda ya kati, wakati kanda ya mashariki vituo vilivyoongezwa ni pamoja na pwani na Dar es salaam.
"Katika kuboresha huduma katika kituo cha uwekezaji ofisi imeanzisha mfumo uitwao (one stop facilitation Center) ndani ya ofisi zetu ambapo mfumo huo utatoa huduma za usajili wa makampuni pamoja na kodi" amesema Mwambe.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji John Mnali amesema miundombinu kama umeme barabara ni changamoto kwa wawekezaji na serikali inaendelea kushughulikia ili kuboresha mazingira ya wawekezaji waendelee kuongezeka siku hadi siku.
Aidha amesema Serikali inaendelea kupatia ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokuwa vikwazo kwa wawekezaji na inatoa utaratibu wa upatikanaji wa Ardhi kwa wawekezaji wengi jambo ambalo litapelekea kukuza uchumi wa kati pamoja na uchumi wa viwanda.
Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi na Mamlaka zote Nchini,kujenga uelewa,kutoa miongozo na kusimamia Ujenzi wa Viwanda Nchi nzima katika mikoa na Wilaya zote.
Aidha amesema Serikali inaendelea kupatia ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokuwa vikwazo kwa wawekezaji na inatoa utaratibu wa upatikanaji wa Ardhi kwa wawekezaji wengi jambo ambalo litapelekea kukuza uchumi wa kati pamoja na uchumi wa viwanda.
Kituo cha Uwekezaji kinaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi na Mamlaka zote Nchini,kujenga uelewa,kutoa miongozo na kusimamia Ujenzi wa Viwanda Nchi nzima katika mikoa na Wilaya zote.