Kijana apata fahamu kabla ya madaktari kumuua Marekani

Trenton McKinley,Haki miliki ya pichaJENNIFER REINDL/FACEBOOK
Image captionMvulana wa miaka 13 katika jimbo la Alabama nchini Marekani alipata fahamu baada ya wazazi wake kutia saini stakhabadhi za kufadhili viungo vyake.
Mvulana wa miaka 13 katika jimbo la Alabama nchini Marekani alipata fahamu baada ya wazazi wake kutia saini stakhabadhi za kufadhili viungo vyake vya mwili.
Trenton McKinley aliugua tatizo la ubongo alipoanguka katika trela ya gari ambayo ilimuangukia katika kichwa chake.
Madaktari waliambia wazazi wake kwamba hawezi kupona na kwamba viungo vyake vilikuwa vikifanana na vile vya watoto wengine watano ambao walihitaji kupandikizwa.
Siku moja kabla ya maisha yake kuondolewa , Trenton alionyesha ishara za kupona. Fuvu la kichwa la kijana huyo lilivunjika mara saba katika ajali hiyo mjini Alabama mnamo mwezi Machi.
Kulingana na mamake, Reindl , Trenton amefanyiwa upasuaji akiugua tatizo la figo na moyo.
Wakati moja , bi Reindl aliambia CBS News kwamba alikubali kutia saini stakhabadhi za kufadhili viungo vya mwili , kwa mujibu wa bi Reindl akikumbuka vile mwanawe alivyopata fahamu mwezi Machi.
Siku iliofuata alitarajiwa kufanyiwa kipimo cha mwisho cha ubongo wake ili kumsaidia kufa, lakini amini usiamini kijana huyo alionyesha ishara nzuri za kutaka kuendelea kuishi.
Trenton McKinley,Haki miliki ya pichaJENNIFER REINDL/FACEBOOK
Image captionTrenton anasema kuwa hakumbuki chochote baada ya ajali hiyo
Trenton sasa anaendelea kupona polepole .
"Nilijigonga kichwa na sakafu na baadaye trela ikaniangukia kichwani. Baada ya hilo sikumbuki chochote'' , alisema.
Bado ana maumivi na ameshtuka. Na atahitaji upausuaji ili kuunganisha fuvu lake la kichwa.
''Amekuwa akitembea na kuzungumza hata kusoma na kufanya hesabati'' , bi Reindl alisema akitarajia kuwa miujiza.
Trenton mwenyewe aliambia WALA alidhania kwamba alikuwa mbinguni wakati alipokosa fahamu.
''Nilikuwa katika uwanja ulio wazi nikitembea'' , alisema kijana huyo.
''Hakuna maelezo isipokuwa Mungu pekee''.
Familia imeanza kuchangisha fedha katika mtandao wa Facebook ili kumsaidia kimatibabu

Related

KIMATAIFA 6044640157057824056

Post a Comment

emo-but-icon

item