JKT yaonyesha Ubabe wake tena wa Ngumi Meya Mwita Cup

MASHINDANO ya ngumi kombe la Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita yamemalizika jana huku mabingwa watetezi ambao ni mabondia wa  JKT waliibuka kidedea na hivyo kuchukua kombe kwa mara ya pili mfululizo.
Mpambano huyo wa aina yake ulimalizika jana katika uwanja wa ndani wa Taifa ambapo Meya Mwita alikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza ambayo ni Makao makuu ya JKT, iliyopata pointi  10.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo  ni timu  ya mkoa wa Dar es Salaam ( mzizima) chini ya Kocha  Haji Fera ambapo walipata pointi nane,  huku  mshindi wa tatu  ikiwa ni Halmashauri ya   Manispaa ya Ubungo.

Awali Meya Mwita alisema kuwa michezo ni jambo muhimu kutokana na kwamba huwezesha vibaya kupata ajira, kuwaweka  pamoja na kwamba katika uongozi wake jijini hapa atahakikisha mchezo wangumi unapewa kipaumbele.
Meya Mwita alifafanua kuwa kwakipindi kirefu mchezo huo ulisahaulika na kwamba jiji limeanza kujenga kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mashindano hayo.

"Michezo ni ajira, michezo ni burudani, utakumbuka juzi hapa tumefanya vibaya kwenye jumuiya ya madola, mtakubaliana na mimi kwamba mchezo huu wa ngumi ulisahaulika, lakini uliwahi kutuletea sifa kubwa katika nchi yetu.
Sasa nijukumu letu kama viongozi, kuungana na wadau wamichezo kufanya maandalizi ya kutosha ili turudi kwenye mstari tuliokuwa mara ya kwanza"alisema Meya Mwita.
Hata hivyo Meya Mwita aliwapongeza mabodia walioshiriki kwenye mpambano huo nakuahidi kuwa atatua changamoto zinazo wakabili sambamba na kuhakikisha kuwa wanashiriki kwenye mashindano nje ya nchi.


Related

michezo 8769700315043651014

Post a Comment

emo-but-icon

item