GSM MALL yatangaza vunja bei katika msimu huu wa sikukuu ya idd

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/ggsm-mall-yatangaza-vunja-bei-katika.html

KAMPUNI Gsm Mall, leo imetangaza bei za bidhaa zake ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Msimu huu wa Mfungo wa Ramadhani katika kuelekea sikukuu ya Idd.
Akizungumza na waandishi wa habri hii leo, Meneja Masoko wa Gsm Mall, Farida Rubanza, amesema katika kuwajali wateja wake wameona ni vyema wakaja na bei nafuu ili kila mtu afurahie sikukuu ya Idd vizuri kwa kununua bidhaa mbali mbali ikiwemo Nguo pamoja na Fanicha.

Amesema kuwa kila duka litakuwa linatoa ofa ya Nguo mbili kwa gharama ya Shilingi Elfu 20, huku akiendelea kufafanua zaidi kwamba Kampuni yao ina Maduka ambayo yanakidhi mahitaji ya Familia nzima.



Amewaomba wateja wote kukaribia kwani bidhaa zao ni za bei ya chini na nafuu ambazo zimezingatia viwango vya ubora.


Mbali na bidhaa hizo pia wamezindua Promosheni za katika Mitandao ya kijamii ijulikanao kama ""Like My Selfiegsm""huku akisema kuwa maduka kama vile Msasani, Pugu, Baby shop na Splash iliyopo Milimani City unaweza kupiga picha na kutagi katika mtandao wake na kama mtu atafanikiwa kupata watembeleaji kuanzia 100 atajinyakulia kiasi cha pesa Tasiimu Shilingi Laki Moja na kila Jumapili watagawa zawadi kwa washindi.


""Zawadi hii sio kwa Mtu mmoja mmoja bali hata kwa wale wateja watakaopiga picha pamoja na Familia zao nakufanikiwa kupata watemebeleaji kuanzia mia moja nao tutawapatia a zawadi ya Nguo za Watoto Wakike na Wkiume ""amesema Rubanza

Amewatakia heri na baraka kwaniaba ya Uongozi wa Gsm Mall kwa Waislamu wote waliokatika mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwakaribisha sana katika manunuzi yao.-

