Meya Mwita ashangaa watu wa Kisiwa Cha Mayotte wakizungumza Kiswahili.

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa.

Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.

Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda  wa Mayotte Nchini Ufaransa Hamidani Magoma akimuelekeza jambo kwenye kwenye dokomenti Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita walipomtembelea ofisini kwake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya biashara jijini hapa.

Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda Hamidani Magoma mwenyemiwani  walipokutana katika ofisi za Mastahiki Meya jiji.

Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda  wa Mayotte Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili.

Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita watatu kulia mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Kisiwa Cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa walipomtembelea ofisini kwake.


“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili, hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha yetu” amesema Meya Mwita.


Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.

Imetolewa leo Desemba 1 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.

Related

habari 5648486238819792156

Post a Comment

emo-but-icon

item