Dewji aibuka kidedea uwekezaji Simba

Bilionea Mohammed Dewji, amepita katika mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Sh bilioni 20.
Dewji amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Sh bilioni 20 kupata hisa asilimia 51.

Hata hivyo, baada ya mchakato huo makubaliano yalikuwa ni hisa 49 anazoruhusiwa kuchukua kwa kitita hicho cha Sh bilioni 20.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo zabuni, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” alisema.


Mkutano huo wa wanachama bado unaendelea Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Related

michezo 6669016480612701743

Post a Comment

emo-but-icon

item