Almasi kubwa ya karati 709 ambayo ilipatikana nchini Siera Leona imeuzwa kwenye soko la mnada mjini New York kwa dola milioni 6.5.
Laurence Graff, mwenyekiti wa Graff Diamonds, ndiye aliinunua almasi hiyo kwa jina "peace diamond" kwenye mnada siku ya Jumatatu.
Serikali ya Sierra Leone ilikataa bei ya dola milioni 7.8 kwenye mnada wa awali.
Serikali sasa inatarajiwa kutumia pesa hizo kuboresha hali ya maisha katika kijiji cha Koryardu ikiwemo miradi ya maji, umeme, barabra na huduma za afya.
Mapema bei ya dola milioni 7.8 ilikataliwa na serikali wakati jiwe hilo liliweka kwenye mnada mjini Freetown baada ya kusema kuwa bei hiyo ilikuwa ya chini mno.
Almasi hiyo iliyotajws kuwa ya 14 kwa ukubwa kuwai kupatikana duniani, ilikabidhiwa serikali ya Sierra Leone mwezi Machi baada ya kupatwa na Emmanuel Momoh ambaye ni muhubiri wa kikiristo.