Siri ya Yanga kuongoza mzunguko wa kwanza yajulikana
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/siri-ya-yanga-kuongoza-mzunguko-wa.html
Ligi Kuu ya Vodacom imesimama kwa zaidi ya wiki mbili kupisha michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza Disemba 03, nchini Kenya.
Shirikisho la soka nchini (TFF) limesimamisha ligi ili kuwapa nafasi wachezaji waliochaguliwa katika timu zao za Taifa kwenda kushiriki michuano hiyo bila kuziathiri timu zao.
Yanga ina jumla ya wachezaji tisa walioitwa timu za Zanzibar, Tanzania Bara na Zimbabwe.
Michuano hiyo inatarajiwa kukamilika Disemba 17.
Baada ya kukamilika kwa michuano hiyo Yanga itasafiri jijini Mwanza kucheza na Mbao FC kisha kurejea jijini Dar es salaam kukamilisha ratiba ya mzunguuko wa kwanza kwa kuzivaa Mwadui FC, Ruvu Shooting na Azam FC kwenye dimba la Uhuru.
Yanga itakuwa na nafasi ya kumaliza mzunguuko wa kwanza ikiwa kileleni kama mkufunzi wake Mwalimu George Lwandamina atazichanga vizuri karata zake.
Tofauti na Yanga itakayokuwa na mchezo mmoja tu mkoani, kisha kurejea jijini Dar es salaam kumalizia mechi zake zote zilizobaki, Simba itakuwa na michezo miwili nyumbani na ugenini ambayo hata hivyo mpangilio wake waweza kuwa changamoto kwao.
Kwanza itasafiri mkoani Mtwara kuivaa Ndanda FC kisha itarejea jijini Dar es salaam kuivaa Singida United.
Baada ya mchezo dhidi ya Singida United itatakiwa kusafiri kwenda Kagera kuivaa Kagera Sugar kisha itarejea tena jijini Dar es salaam kumalizia mchezo wa mwisho mzunguuko wa kwanza dhidi ya Majimaji.
Kocha George Lwandamina ametoa mapumziko ya wiki moja kwa wachezaji wake ambapo wale ambao hawatakuwa na majukumu kwenye timu za Taifa wanatarajiwa kurejea mazoezi Jumatatu ijayo.