NAMNA YA KUYAREJESHA MAPENZI YALIYO KATIKA .
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/namna-ya-kuyarejesha-mapenzi-yaliyo.html
NA
ISSA RAMADHANI.
Karibu Unapoingia
katika mahusiano ni kama unakuwa umeingia katika maisha mapya, mambo ambayo
umezoea kuwa unafanya kila siku katika
maisha yako kabla, huenda mengi hutokiwi kuyafanya.Kuwa katika mahusiano na mtu(mpenzi) kunakupelekea katika dunia
nyingine tofauti na ya mwanzo ,Huwezi kuwa kama awali kama ulikuwa na mazoea ya kukaa nje au kurudi muda unaotaka mwenyewe
hadi saa sita usiku isiwezekana, mazoea
yaliyoptza na akina amina au issah.
Mapenzi si
jela ila ni suala linalokupa mpaka wa kufanya baadhi ya mambo kwa mpenzi wako
bila kupata ruhusa na kuwahi kurudi nyumbani mapema, kwenda na mabadiliko kuwa
mnashauriana na mpenzi wako baadhi ya mambo,ushauri na kupanga mipango ya
familia yenu kuwa na mapenzi ya dhati kati yenu siku zote.
Sababu zinazochangia wapenzi ,wananoda wakaachana
, kwa ufupi tabia kutofautiana kati yao
mfano mme mlevi na kumpga mke kila siku bila sababu, wakati mwingine hakuna
maelewano ndani ya nyumba,michepuko na
kuchokana kimapenzi hatimaye kunyimana
unyumba na nyinginezo.
Swali je
wajua namna ya kuyarejesha mapenzi yaliyokatika au kuisha ? Ungana name katika
makali hii nikujuze na kubadilshana
mawazo, Baadhi ya njia sahii kurejesha tena mapenzi na mwenza wako au
mchumba katika mahusiano tenu na mpenzi
wako kurudiana kwa kuangalia maeneo uliyokosea
wewe au mpenzi wako na kufanya haya.
Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye kitu
chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote kwa
pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda sawa
kwa upande wao. Na ndio sababu hata ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu
yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;
TABIA YA KUWA NA UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwa waliopo katika mapenzi, uongo wa aina yoyote si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
KUWA NA USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.
ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi.
Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.
SUALA LA DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmoja wapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa linapokuja suala la doa au kuishi na Mtu, Kwetu Sie wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo wa wwanamke kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.
KUWA MROPOKAJI/ASIYE MSIRI.
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni mropokaji na huna ‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda kusimulia.
Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda mtaani unakuta kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo vile, hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.
SUALA LA TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa naye basi usiwe na tamaa kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza kuku-cost hapo baadae.
KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao na vyombo mbali mbali vya habari.
Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi wake.
Halo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
ReplyDeleteBarua pepe: dawnacuna314@gmail.com