Chanzo na namna ya kujinasua na mapenzi ya kulelewa(Serengeti Boys)
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/chanzo-na-namna-ya-kujinasua-na-mapenzi.html
NA
ISSA RAMADHANI.
KARIBU
mwanandoa
mwenzangu kwenye safu ya mahusiano,tubadilishane
mawazo na kujuzana mambo kadhaa kama wanandoa au mchumba. Leo tutazungumzia umuhimu
wa tendo la ndoa kwa wanandoa na watarajiwa pekee.
Chanzo au sababu
zinazopelekea vijana wa wenzangu wa kiume wengi kupenda kulelewa kimapenzi na wanawake wakubwa maarufu
(Mijimama) waliowazidi umri na
wenyeuwezo kifedha hali hii ushawishika kwa uraisi, kuwa katika mahusianon ya
kimapenzi na wengine hufunga ndoa.
Kadri siku hadi siku, wanandoa au vijana wengi wamekuwa wakijuhusisha kuwa na mapenzi
na mjimama, (Serengeti boy ) vijana wakiume na kwa hakika tabia hii inakua kwa kasi kubwa
mno na kuona kama jambo la kawaida, ingawa wanasaikolojia wanasema tabia hii ya kupenda kitonga au kushuka katika kupata
kipato na kujikimu mahitaji yao ya
kimwili,fedha na mengineyo. Ni tabia mbaya san na haifai katika jamii , mila na
tamaduni zetuhazipendezi.
Hali hii imekuwa ikiwafanya hasa vijana wengi kuwa
na mawazo hasi au uvivu, kwamba kulelewa na mijimama ni sawa. Bila kujali
ameolewa au laha, na hivyo pia kwa mabinti wadogo kuwa na vibabu .
Swali
la kujiuliza ni kwamba, kwa nini Serengeti boy hupenda kulelewa kaitika mapenzi
na huwa ni wanawake wakubwa(mijimama) yenye fedha zao waliowazidi umri mara 4 au 7 bila kujali ameolewa au ana maambukizi huwa
hawa angalii hujali mapenzi na pesa.
SABABU
;
Tamaa
za kutaka kuwa na maisha mazuri, Tabia hii ya baadhi
ya vijna kupenda kujirahisisha au njia za mkato katika utafutaji wa ridhiki (maisha) , hujikuta wakiangukia
mikononon mwa mijimama wenye uwezo kifedha na kulelewa katika maisha ,na kupata kila
ancho hitaji bila kufikiria madhara au matatizo baadeye mbeleni mfano
kuambukizwa na kufa ugonjwa wa ukimwi, migogoro kati ya familia yake na marafiki.
Hapa huwa hamna mapenzi ya dhati kabisa ni kama utumwa wa mapenzi tu kwa kijana
maarufu (Serengeti Boys) wa kiume.
Uhitaji
wa mtoto,Wakati mwingine hii ni sababu kwani kijana
anshawishiwa na jimama kwa kila mbinu na zawadi, lengo ni kutaka mtoto na
baadaye kuachana hapa ndipo kijan anapata matatizo kwa kudai mtoto wake na
kutoelewana na jimam. Huenda jimama mme wake
hasababashi au haja yake ni kuzaa mtoto na Serengeti boy amtie mimba,
baadaye anaachana nae. Wakati mwingine husabisha mtafaruku na kijana kupata
matatizo.
Malezi
mabaya ya wazazi, Ni kwa sababu Baadhi ya wazazi au
walezi tunalea watoto vibaya ,Hii nchi
imekosa msingi bora wa kuwafunza watoto
shuleni kuanza kujitegemea katika
kuwafundisha shughuli ndogondogo na wazazi pia tumeiachia serikali. kama mzazi
unatakiwa kumuandaa mwanao tabia ya kujifunza na ajitegemee, awe na njia mbadala katika maisha,
asifikie hatua ya kusema kwamba siwezi kufanya
hiliau lile mfano, kama akishindwa kuendelea na shule awe na ujuzi wa
kazi za mikono kulima bustani,ubunifu wa kusuka mkeka, ufundi wa aina yeyote.
Ili asiwe na mawazo mgando na hasi kuwa kulelewa na jimama(SUGAR MUMMY)
ni dili.
kufuata
mapenzi / tama za kimwili , Hapa vijan wengi
hushawishiwa na mijimama(Shugar Mummy) kufanya mapenzi naye , Huenda jimama mme
wake hapigi game kamili na anaamini kijan bado damu inachemka napiga game
kamili na anamlizisha kimapenzi na kuwa wapenzi na kijana kupewa kila anachotaka
bila kujali kuambikizwa magonjwa ya
ziana na mengine ,Licha ya kukupatia
pesa na mhitaji ya kimwili na mengineyo.
Msukumo
wa makundi mabaya, Kuna baadhi ya makundi katika jamii ambayo vijana wa kiume (Serengeti
Boys ) wana tabia hii ya kujishikiza kwa mijimama wenye maisha mazuri pia
huwashawishi huwashawishi na wenzao
ambao hawna mpango, mawazo kuwaja ujinga
ili kujipatia na kutimiza mahitaji yao katika maisha.Tabia hii mjini
inakomaa kila siku vjiana hawajishughuishi kabisa.
Ugumu
wa maisha na ukata, ukosefu
wa ajira na kukata tamaa ya maisha pia kukosa ubunifu na njia ya kipato kwa
ufupi umasikin ni sababu kubwa sana inayopelekea vijana kulelewa
na mijimama kuwa wapenzi wao.
vijana wengi tunamitizamo hasi kuwa wamama(mijimama) wanalea kutokana na kuwa ameshaanza kufanya kaz kwa miaka zaidi ya 10 na ana kipato au maisha mazuri hivo amechuma. Wakati mimi kijana(Serengeti boy) sina kitu naangaika na mtaani maisha yamezid kuwa magumu kila siku vitu vinapanda bei. Na kulalamika umasikini.
Namna
ya kujinasua na mapenzi ya kulelewa (Serengeti Boys)
Suluhu ,
Hapa napenda nitoe ushauri kwa kijana
mwenazangu ni kujituma kwa kufanya kazi zako za utafutaji kila siku ili kufikia
malengo yako. Achana na tabia ya uvivu
kuwa na ratiba nzuri katika shughuli zako ,Hii itasaidia kuwa bize na kuepuka makundi na visahwishi ,
makundi mabaya na kuwakataa mijimama wakikutongoza na kukushawishi kwa nguvu kabisa na usipende
mteremko pamana na hali yako kijana , hii ni kwa wote kiume na wakike.
Ushauri.
Muombe
mungu akupe mmke mwema , kuliko kulelewa na jimama tajiri na anakunyanyasa,
kukubaka katika mapenzi. Huu ni utafiti niliufanya kwa kuwahoji vijana wa kiume
na wandoa , wazazi pamoja na wahenga.Ni vema kufatuta mpenzi au mchumba unaye mpenda kwa dhati na kuanzisha familia
yako.
|