Malalamiko ya Mbea City yatua bodi ya ligi

KLABU ya Mbea City imekata  rufaa bodi ya ligi ya kutaka kusikililizwa dhidi ya maamuzi ya mechi yao na Simba SC jumapili ya tarehe 5 November 2017. Rufaa hiyo inaelezea kutoridhishwa na goli walilofungwa dakika ya 7 na Shiza Kichuya. Wanalilalamikia kwamba ni goli la kuotea.
Image result for mbeya city vs simba jana
Uongozi wa timu ya Mbeya City umeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulalamikika kutotendewa haki katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.

Mbeya City ilichapwa 1-0 Jumapili na Simba, bao pekee la Shiza Ramadhani Kichuya katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema kwamba uchezeshaji wa refa Ahmed Kikumbo aliyesaidiwa na Omar Juma wote wa Dodoma na Michael Mkongwa kutoka Njombe haukuwa wa haki kwa mujibu wa sheria 17 za soka.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

michezo 1763855694460726753

Post a Comment

emo-but-icon

item