Best Naso awaumbua wanaomuita wa Kijijini

MSANII  wa muziki Bongo, Best Nasso amesema si sawa kuitwa msanii wa kijijini kwani hata mjini anafanya vizuri pia.
Image result for BEST NASSO

Muimbaji huyo amesema kuwa bado anaamini katika uwezo wake wa kimuziki ila suala la management ndilo limemkwamisha.
“Kilichokuwa kinanikwamisha ni kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa na management na sasa hivi nipo nje ya management ndio utofauti mkubwa lakini Nasso ni yule yule na bado anafanya ngoma kali, nishakuwa msanii wa mjini” amesema Best Nasso.
“Sitaki kuamini mimi ni msanii wa kijijini pake yake lakini kama mjini wananifahamu mimi ni msanii wa kote kote, lakini kijijini nimekuwa na nafasi kubwa na mshindo mkubwa kuliko town” ameongeza.
Kwa sasa Best Nasso anatamba na ngoma yake mpya ‘Tumenatana’.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

burudani 4140825506194403353

Post a Comment

emo-but-icon

item