Waziri Mjaliwa atoa neno akikabidhi tuzo za Washindi wa Kusoma na Kuhifadhi Quruan Afrika

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/waziri-mjaliwa-atoa-neno-akikabidhi.html
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Amezitaka taasisi za dini kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza elimu nchini.
"Napenda kuwaambia ndugu zangu Waislamu, tofauti za kidini hazikuanza leo, zilikuwepo tangu zamani hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu likapewa nafasi na dini zote" amesema Majaliwa.
Mashindano ya mwakani, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
"Wakati niko hapa mbele nimepokea simu kutoka kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli akaniuliza hao wote walio jana uwanja ni Waislam? nikamwambia ndiyo, akauli za tena nawewe ni mgenirasmi miaka miwili mfululizo? Nika sema ndiyo, akasema mwakani mimi nitakuwa mgeni rasmi na huyo shekh wa msikiti wa Maka nitamleta nitakuwa naye hapo" amesema Majaliwa.
Pamoja na hayo Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi zawadi kwa Washindi wa mashindano hayo.
Mshindi wa juzuu tatu kutoka AL-HIKIMA Salah, Yasir juma amepata zawadi ya 800,000
Mshindi wa juzuu tano kijana kutoka madrasa ya alhkima Mohamed. Ahmed zawadi milioni 1.
Mshindi juzuu kumi Bilal Saleh Abdalah zawadi milioni 1.2
Mshindi wa Juzuu 30 ni Mbwana Dadi Abdalah kutoka pemba kaskazini Zanzibar katika Taasisi ya AL-HIKIMA zawadi milion 15
Baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Waziri wa Dini kutoka Saudia Arabian, Dr Saleh bin Mohamad bin Abdullah Azizi Alshekh.