TPSF kushirikiana na Wizara ya Elimu waja na mkakati wa kukuza ujuzi ili kusukuma maendeleo ya uchumi

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/tpsf-kushirikiana-na-wizara-ya-elimu.html
TAASISI ya Sekta binafsi Tanzania ( TPSF) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na teknologia wamezindua mkakati wa kitaifa wa ukuzaji na uendelezaji ujuzi wenye lengo kutoa ushindani wa kusukuma maendelea ya uchumi na kijamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia, Profesa James Mdoe alisema kuwa ili kutekeleza mkakati huo,Tpsf imepewa jukumu la kuratibu na kuanzisha mabaraza ya kisekta ya kukuza ujuzi.
"Mabaraza haya yana umuhimu mkubwa sana kwa sababu yatakutanisha pamoja wadau wa sekta husika ili kuijadili na kukubaliana maeneo ya kipaumbele yanayohitji kujengewa uwezo na kutengeneza mipango mkakati ya kisekta"alisema Prof Mdoe.
Aidha alisema katika kutekeleza mkakati huo wa kitaifa wa miaka 10 ambapo umezinduliwa 2016 hadi kufikia 2026 wa kuendeleza na kukuza ujuzi pia wameanzisha mradi wa miaka 5 ambapo Serikali imepata mkopo wa bei nafuu kutoka benki ya dunia dolla za kimarekani 250 ambapo hadi sasa wamechukua dolla million 120.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tpsf Godfrey Sembei alisema kuwa,Sekta binafsi nchini zimekua mstari wa mbele katika kusaidia Serikali katika masuala ya Ujuzi pamoja na kuajiri vinaja wenye ujuzi, ambapo alisema kuanzia wikin ijayo wataanza na baraza mawili hadi kufikia mwezi wa sita yatakuja yamekamilika.
Alisema kuwa, mbaraza hayo yatakua na kazi ya kuangulia na kupata watu wenye ujuzi wanaohitajika kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo 2025, ambapo yatasimamiwa katika, sekta zilizopewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya kilimo, Utalii, UsafIrishajI, Nishati na Habari mawasiliano na teknolojia na Ujenzi.