Shambulio la kisu Paris: Mshukiwa ni mzaliwa wa Chechnya'



Ramani ya Paris kulikotokea shambulio
Image captionRamani ya Paris kulikotokea shambulio
Mshukiwa wa shambulio baya la kisu katikati mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris siku ya Jumamosi jioni, alizaliwa mwaka 1997 katika iliyokuwa jimbo la Urusi, Chechnya. Hayo ni kwa mjibu wa duru za idara ya mahakama.
Mshambuliaji huyo alimuuwa mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 29 na kuwajeruhi watu wengine 4 katika eneo lenye shughuli nyingi ya Wilaya ya Opéra, kabla ya kupigwa risasi na kuuwawa na maafisa wa polisi.
Mashuhuda wamesema kuwa, walimsikia mshukiwa huyo akifyoka "Allahu Akbar" yaani (Mungu ni Mkuu).
Kundi linalojiita Islamic State (IS), baadaye lilisema kuwa mmojawepo wa "askari wake" alitekeleza shambulio hilo.
Kwa muda sasa, Ufaransa imekuwa katika tahadhari ya kutokea kwa misururu ya mashambulio ya kigaidi.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, zaidi ya watu 230 waliuwawa na wanajihad wa itikadi kali wa kundi la wapiganaji wa IS.

Related

KIMATAIFA 2222813400584128178

Post a Comment

emo-but-icon

item